Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Saturday, June 19, 2021

Mhe. John Mrosso Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani amefunga rasmi mafunzo elekezi kwa majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Zanzibar

 

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. John Mrosso akifunga rasmi Mafunzo Elekezi kwa Majaji Wapya wa Mahakama ya Tanzania na Zanzibar yaliyokuwa yanafanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 

 Waheshimiwa Majaji wa Mahahakama Kuu wakifuatilia tukio la ufungaji wa Mafunzo Elekezi yaliyofanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 31 Mei na kufungwa tarehe 18 Juni, 2021 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.



1. Waheshimiwa Majaji wa Mahahakama Kuu wakifuatilia tukio la ufungaji wa Mafunzo Elekezi yaliyofanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 31 Mei na kufungwa tarehe 18 Juni, 2021 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.


1. Waheshimiwa Majaji wa Mahahakama Kuu wakifuatilia tukio la ufungaji wa Mafunzo Elekezi yaliyofanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 31 Mei na kufungwa tarehe 18 Juni, 2021 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.


1.     Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. 



1.     Mhe. John Mrosso Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama wilayani Lushoto. Kuliani Mhe. Salum Masatti Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani na Mkurugenzi wa Mafunzo Elekezi ya Majaji. Kushoto ni Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jajiwa Mahakama ya Rufani na Mkuuwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto









1.     Mhe. John Mrosso Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbalimbali na Washiriki wa Mafunzo Elekezi. Kulia ni Mhe. Salum Masatti Jajiwa Mstaafu wa Mahakama ya Rufani na Mkurugenzi wa Mafunzo Elekezi ya Majaji. Kushoto ni Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto








Tuesday, June 1, 2021

TIMIZENI MAJUKUMU YENU KWA KUFUATA SHARIA: JAJI MKUU







Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, amewataka majaji

walioteuliwa na kuapishwa hivi karibuni kumwogopa Mungu na kutimiza

majukumu yao kwa kufuata Sheria, Katiba na kwa kuzingatia maadili na

viapo vyao.

Mhe. Jaji Mkuu alitoa wito huo Mei 31, 2021 alipokuwa akifungua mafunzo

elekezi kwa majaji hao, saba wa Mahakama ya Rufani, 21 wa Mahakama

Kuu ya Tanzania na watatu kutoka Mahakama Kuu ya Zanzibar,

yanayofanyika katika Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Aliwakumbusha majaji hao kuwa katika Karne ya 21, idadi ya sheria

zimeongezeka huku kasi za marekebisho ya sheria hizo nazo ikiwa

zimeongezeka, hivyo Jaji anapaswa kujiridhisha kama kuna marekebisho

ya sheria inayohusu jambo lililo mbele yake.

“Tukumbuke kuwa sheria zimejiingiza sana katika shughuli za kila siku za

kiuchumi, kibiashara, kijamii, kisiasa na kugusa maisha ya kawaida ya

wananchi wengi zaidi. Kwa hiyo, majaji, kama  watafsiri wa mwisho wa hizo

sheria nyingi, mnatakiwa kuwa watu wa Mungu ili kuhakikisha kuwa

mamlaka ambayo wananchi wamejibakizia kwa mujibu wa Katiba

hayaingiliwi na Mihimili mitatu ya Dola,”alisema.

Jaji Mkuu alibainisha kuwa utashi wa nafsi ya jaji, ubinadamu wake na

ubuntu wake lazima uwe wenye kumwogopa Mungu kwa kutambua kuwa

ingawa Katiba na Sheria zimewapa mamlaka makubwa na ya mwisho

katika jambo la utoaji haki, lazima watambue kuwa kuna Mwenyezi Mungu

wa kumwogopa na kuna ubinadamu na ubuntu wa kuheshimu.

“Vinginevyo unaweza kutumia sheria kufifisha haki ambazo wananchi,

kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, wamejiachia wao wenyewe.

Katiba ni sauti ya wananchi. Katiba imefafanua wananchi wamekopesha

mamlaka gani kwa mihimili ya Dola,” alisema.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, wananchi wamebakisha mamalaka yote ambayo

majaji hawatakiwi kuyaingilia kupitia sheria zilizotungwa na Bunge na

kupitia maamuzi ya kimahakama na utekelezaji wa shughuli za serikali.

“Ukweli kuwa wananchi wamebaki na haki zao za msingi umebainishwa

katika utangulizi wa misingi ya Katiba inayotukumbusha sisi majaji na


vingozi wote wa umma kuwa tumekopeshwa mamlaka chache ambayo

tunapaswa kuyatuma kwa manufaa ya wananchi,” alisema.

Prof Juma amekishukuru Chuo cha Uongozi wa Mahakama, kupitia Mkuu

wa Chuo hicho, Dkt Paul Fauatine Kihwelu, kwa kuandaa mafunzo hayo ili

kuwatayarisha majaji hao kufanya kazi ya ujaji wa Mahakama Kuu na

Mahakama ya Rufani kwa ukamilifu.

Aliwakumbusha Majaji hao pia kuwa mafunzo hayo elekezi

yatawatayarisha kuwa sehemu ya Dira na Mpango Mkakati wa Mahakama

na hivyo kuwa sehemu  muhimu ya nguzo za mpango mkakati wa

mahakama na sera mbali mbali zinazohusu mahakama.

“Lengo hapa ni kuhakikisha kuwa mnavuka kwa haraka kipindi cha

kujifunza kazi za ujaji na mnaanza mara moja majukumu yenu ya ujaji

mahakamani mara baada ya mnafunzo haya elekezi,” alisema Jaji Mkuu.

Alibainisha pia kuwa Mahakama ya Tanzania inatambua kuwa kadri dunia

inavyopitia mageuzi makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia kupita Mapinduzi

ya Nne ya viwanda, hugusa sana taratibu zilizopo za utoaji haki.

Jaji Mkuu alieleza kuwa kama majaji na mahakimu hawatapata mafunzo

endelevu mara kwa mara watajikuta wanaachwa mbali sana na mageuzi ya

kimaboresho. Hivyo, alisema kuwa Uongozi wa Mahakama ya Tanzania

umetoa kipaumbele kwa mafunzo elekezi na endelevu kwa majaji na

mahakimu ili kuboresha ufanisi, ujuzi, weledi na uwazi.

“Ni matumaini yangu kwa mafunzo haya elekezi yatawasidia kujenga

misingi ya positive attitude (Mtazamo chanya). Mada Mtakazopata katika

maeneo ya maboresho yatalenga kuwajengea mitazamo ya kimaboresho

na kuondoa negative attitudes (Mitazamo Hasi),” alisema.

Jaji Mkuu pia aliwakumbusha Majaji hao kwa ni viongozi katika nchi

maskini yenye wananchi wenye matarajio kuwa kazi ya viongozi ni

kuwaboreshea maisha, husuani utoaji wa haki. Alibainisha kuwa yapo

maeneo mengi ambayo sifa za uongozi za kila mmoja hujipambanua

wakati wa kutoa maamuzi.

Alisema kuwa kazi kubwa ya Jaji ni kusikiza na kupata ushahidi au

kusikiliza hoja ili zimsaidie kutumia sheria na kufikia uamuzi.


“Kumbukeni kuwa kiongozi mzuri mahakamani ni yule anayehakikisha

mahakama yake inatambua kuwa mwananchi aliye mbele yake ana haki

zake zote za msingi kwa mujibu wa Katiba, ikiwa pamoja na haki ya

kusheshimiwa na utu wake kuthaminiwa,” alisema.

Kuhusu maadili, Jaji Mkuu alisema kuwa uadilifu na maadili mema

husafisha nafsi na kuwawezesha kufanya kazi kwa kuzingatia Katiba na

masharti ya viapo vyao.

Alibainisha kuwa  kunapotokea ukiukwaji wa sheria watu wengi hukimbilia

kudai sheria mpya au marekebisho ya sheria iliyopo na kusahau kuwa

sheria sio mbaya, bali nafsi, maadili na hata tabia za wanaotekeleza sheria hizo ndizo mbaya.