Na: Rosena Suka IJA Lushoto
Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amekipongeza Chuo cha Uongozi
wa Mahakama Lushoto kwa kuwaandaa wahitimu kwa kuwajengea ujuzi na maarifa
katika fani ya sheria kwa ngazi za Stashahada na Astashahada.
Mhe. Prof. Juma aliendelea kuwasihi wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kuibadilisha na kuisaidia jamii pale mtakapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo kwani sheria inahusika na haki.
“Nawaomba mkawe watu wa haki na wenye
kiu ya kutenda haki wakati wote katika yote mtakayoyafanya ili jamii ione
utofauti wenu na wengine. Kutenda haki hakusubiri tu hadi uwe mtumishi wa
Mahakama au mwajiriwa. Ni zoezi endelevu kwa maisha yetu”
Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma aliendelea kuwasisitiza wahitimu hao kwa usemi wa kiingereza usemao “Law is not always the problem. Those who implement the law may be the real problem:” na alifafanua kwa kusema kuwa sio mara zote tatizo huwa ni Sheria au kutokuwepo kwa sheria nzuri, bali sheria inaweza kuwa mbaya pale waliopewa dhamana ya kutekeleza sheria ili itimize malengo wanayotarajia kutoka kwa sheria husika. Aliwaomba wahitimu wa Mahafali hayo kuwa wasiwe na tatizo katika utekelezaji wa sheria kwani masomo ya Stashahada ya Sheria na Astashahada ya Sheria waliyopata yamewapa mwanga wa kuelewa Sheria ili kuweza kutumia sheria kutatua changamoto zitakazojitokeza.
“Watanzania wa leo wanaishi katika
dunia inayosukumwa na Teknolojia yenye nguvu kubwa ya Mapinduzi ya Nne ya
Viwanda (4IR). Wahitimu wenye elimu ya ngazi au daraja lolote ni lazima
wahakikishe kuwa elimu waliyopata kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama haitoshi
ni lazima waiboreshe kila siku ili ilingane na mahitaji ya ushindani mkubwa
katika Karne ya 21” alisema
Mhe.
Prof. Juma.
Aidha,
Mhe. Prof. Juma amewasihi Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo, Wahadhiri,
Wakufunzi na watumishi wote wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto,
kujitayarisha na matumizi ya Jukwaa la Ki-elektroniki kutoa mafunzo na
elimu kwa waliopo ndani na nje ya Chuo ambapo itaweza
kutumika sio tu kwa wanafunzi wa Stashahada na Astashahada ya Sheria, bali pia
litatumika kutoa mfunzo Elekezi na
Endelevu kwa Majaji, Wasajili, Naibu Wasajili, Watendaji, Mahakimu na Watumishi
wa kada zote.
Mahafali ya 22 ya IJA yameambatana na ufunguzi wa jengo la bweni la wavulana. Bweni hili lina ghorofa nne na lina uwezo wa kulaza watu 320 na lina thamani ya shilingi za kitanzania billioni 2.6. Ujenzi wa bweni hili ulisimamiwa na Mahakama ya Tanzania katika mpango wa Maboresho ya Mahakama.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis
Juma akitoa hotuba wakati wa katika
Mahafali ya 22 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) leo tarehe 07
Desemba, 2022.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Ibrahim Hamis Juma na meza kuu katika picha ya pamoja na Jumuiya ya wahitimu wa IJA (IJA ALUMN)
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Ibrahim Hamis Juma na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
(IJA).
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.
Ibrahim Hamis Juma na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi Wahitimu wa Stashahada ya Sheria kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
(IJA).
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi Wahitimu wa Astashahada ya Sheria kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akikata utepe kuashiria uzinduzi wa bweni la wavulana Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). Kushoto ni Mwenyekiti
wa Baraza la Uongozi (IJA) na Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, kulia ni Mkuu wa Chuo
cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo.