Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Friday, November 25, 2022

IJA YATOA MAFUNZO ELEKEZI KWA SERIKALI YA WANACHUO

 Na Rosena Suka, IJA

Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo leo tarehe 25 Novemba, 2022 amefungua mafunzo elekezi ya siku moja kwa Viongozi wa Serikali ya Wanachuo wa IJA (IJASO) yaliyofanyika Chuoni Lushoto.

Katika ufunguzi huo  Mkuu wa Chuo amewaeleza viongozi hao  kwamba wanawajibu mkubwa wa kuwahudumia kwa uadilifu wanachuo wenzao  kwani wao ni kiungo  katika kufikisha yale ambayo yanatoka kwenye Uongozi wa Chuo kwenda kwa wanachuo na kutoka kwa wanachuo kwenda kwenye Uongozi wa Chuo.

Mkuu wa Chuo aliwasisitiza viongozi hao wa wanachuo kutumia vikao mbalimbali watakavyokuwa navyo ili kutatua changamoto zao na sio kulalamika au kupeleka changamoto zao kwenye mamlaka zisizohusika. Aliendelea kwa kuwataka viongozi hao kusimamia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kuonyesha mfano bora kwa wanachuo wenzao,

Mkuu wa Chuo, aliwakumbusha viongozi hao kuwa na ushirikiano kati ya wao wenyewe, watumishi wa Chuo na  wanachuo wenzao bila kusahau mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Rais wa Wanachuo, Bw. Meshack D. Tupa alipokuwa akitoa shukrani zake ameushukuru Uongozi wa Chuo kwa kuandaa na kuwapatia semina hiyo elekezi na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na watumishi wa Chuo na wanachuo wanaowawakilisha.

Viongozi hawa wa wanafunzi katika semina hiyo elekezi wamepitisha katika mada mbalimbali ambazo ni Masuala ya Usalama na Maadili, Unyanyasaji na Ukatili wa Kijinsia, Uongozi na Taaluma, Usimamizi wa Rasilimali za IJASO na Usitawi wa Wanachuo.

IJA imekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa Serikali ya Wanachuo mara tu inapowekwa madarakani.


Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akihutubia Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Elekezi ya siku moja yaliyofanyika Chuoni Lushoto

 Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo na wawezeshaji wa mafunzo elekezi. 












Pichani juu ni washiriki wa mafunzo elekezi ambao ni viongozi wa nafasi mbalimbali katika serikali ya wanachuo wakifuatilia mafunzo hayo.

Tuesday, November 8, 2022

IJA YATOA MAFUNZO YA UENDESHAJI WA MASHAURI YA MAKOSA YA KIFEDHA


Mhe. Amiri Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam amefungua mafunzo ya uendeshaji wa mashauri Makosa ya Kifedha (Financial Crimes) kwa maafisa wa Mahakakama 30 katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya siku tano kuanzia leo tarehe 07/11/2022  yameandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Eastern and Southern Africa Anti-Money Laundering Group (ESAAMLG) na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ).

Washiriki wa mafunzo hayo ni Majaji 14 pamoja na Mahakimu Wakazi 26 ambapo kati yao 24 ni Mahakimu Wakazi wa Mikoa Tanzania Bara. Lengo la mafunzo hayo ni kuwafanya washiriki hao waweze kubadilishana uzoefu kwenye maeneo mbalimbali ya sheria za kimataifa na kitaifa za biashara haramu ya wanyamapori, ufadhili wa ugaidi na utakatishaji fedha, kuangalia madhara ya makossa hayo katika taifa na dunia,   urejeshaji wa mali zilizopatikana kutokana na makosa hayo, wajibu wa Maafisa wa Mahakama, wapelelezi na waendesha mashtaka katika uendeshaji wa mashauri yahusuyo makosa hayo n.k.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ofisi ya Mashtaka ya Taifa, Wizara ya Maliasili na Utalii, PPRA, wawezeshaji kutoka mamlaka za wanyamapori za baadhi ya nchi barani Afrika na wawezeshaji wabobevu kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa kwa kundi la kwanza la Mahakimu 40 mwezi Septemba mwaka  huu.

Pichani juu Mhe. Amiri Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam (katikati) alipokuwa anafungua mafunzo ya mafunzo ya uendeshaji wa mashauri Makosa ya Kifedha (Financial Crimes) kwa maafisa wa Mahakama kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ambao wanaonekana kwenye picha za chini.