Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Monday, October 24, 2022

IJA YAENDESHA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA UENDESHAJI WA MASHAURI YA WANYAMAPORI NA MISITU

Na; Rosena Suka  IJA Lushoto

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tanga, Latifa Mansour leo 24 Oktoba, 2022 amefungua mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya makosa dhidi ya wanyamapori ikiwepo ujangiri na makosa yanayohusiana na hayo kwa wadau wa haki jinai. Mafunzo hayo yanaendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania kwa ufadhili wa PAMS Foundation.   

Mafunzo hayo ya siku tano ni mtiririko wa mafunzo mengine kama hayo yaliyofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 10 hadi 14 Oktoba 2022 kwa kundi la kwanza lililojumuisha Majaji wa Mahakama Kuu, Waendesha Mashtaka Waandamizi na Wapelelezi Waandamizi, na kufuatiwa na kundi la pili  la mahakimu, waendesha mashtaka na wapelelezi kuanzia tarehe 17 hadi 21 Oktoba 2022. Hili ni kundi la tatu na mwisho ambalo linashiriki mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ambayo yanahitimishwa.

Akiongea wakati wa ufunguzi Mhe. Latifa Mansour alieleza kuwa mafunzo haya yana lengo la kuwaleta pamoja wadau wa utoaji haki jinai na kubadilishana uzoefu kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sheria za kimataifa na kitaifa za wanyamapori na misitu ikiwemo  upelelezi na uendeshaji wa mashauri ya makosa dhidi ya wanyamapori na makosa yanayohusiana na hayo.

Aidha, Mhe. Mansour aliongeza kwa kusema kuwa mafunzo haya yatawawezesha wapelelezi namna ya kufanya upelelezi kama sheria inavyotaka ili kuwezesha kesi za namna hiyo zinapofikishwa Mahakamani na waendesha mashitaka ziwe na ushahidi wa kutosha na kutokutoa mwanya kwa mtu aliyefanya kosa kukwepa kwa visingizio mbalimbali.

 “Tunaamini kwamba kama Mahakama pamoja na upelelezi itashirikiana na kuhakikisha kwamba hawa watakaobainika na makosa hayo watachukuliwa hatua zipasazo na wanapata adhabu za kutosha ili iwe funzo kwa jamii yote na wale wote wanaofanya biashara hizi haramu.” Alisema Jaji huyo.

Naye mwakilishi wa PAMS Foundation, Bw. Samson Kassala alieleza kuwa  Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali inajishughulisha na masuala ya uhifadhi wa mazingira na usalama wa wanyamapori.   Makao  Makuu ya Taasisi hiyo yako jijini Arusha. Bw. Kassala alifafanua kwa kusema PAMS Foundation imekuwa ikisaidia katika kuwajengea uwezo wale wote walio mstari wa mbele katika kulinda  ulinzi wa maliasili zetu kwa manufaa ya wananchi na vizazi vijavyo kama sheria za nchi zinavyosema.

Bw. Kassala aliendelea kwa kusema kuwa PAMS Foundation imeendelea  kushirikiana na Serikali na wanafanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kwenye maeneo mengi ikiwemo utalii na hasa baada ya ziara ya Utalii (Royal Tour) ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano kati ya IJA na PAMS Foundation ambayo yalisainiwa tarehe 23/06/2022 jijini Dar es Salaam kati ya Mkuu wa Chuo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa PAMS Foundation.



Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Latifa Mansour akiwa anafungua mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya makosa dhidi ya wanyamapori yanayofanyika  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA)



Picha mbalimbali za washiriki wa mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya makosa dhidi ya wanyamapori yanayofanyika  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wakiwafuatilia hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi.





Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Latifa Mansour akiwa katika picha pamoja ya washiriki wa mafunzo ya uendeshaji wa mashauri ya makosa dhidi ya wanyamapori yanayofanyika  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).  Waliokaa kutoka kulia ni Bw. Goodluck Chuwa, Makamu Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, kulia zaidi ni Mhe. Awadhi Mohamed, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Na kutoka kushoto ni Bw. Samsoni Kassala, Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti PAMS Foundation (Mafunzo), kushoto zaidi ni Bw. Elisifia  Ngowi, Mkurugenzi wa Intelijensia na Oparationi  PAMS Foundation.

Wednesday, October 19, 2022

WAJUMBE WA BARAZA LA UONGOZI W CHUO WATEMBELEA BWENI LA WAVULANA IJA

Habari Picha


Muonekano wa mbele wa bweni la wavulana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi 360 

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Dr.  Gerald Ndika (Mwenye Tai Nyekundu) akiwa pamoja na wajumbe wa Baraza la Uongozi na wajumbe wa menejimenti ya Ija walipotembela Bweni la wavulana hivi karibuni IJA


Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Wajumbe wa Menejimenti wakiwa kwenye ziara hiyo




         Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Wajumbe wa Menejimenti wakipita kwenye maeneo                                             mbalimbali ya jengo hilo wakati wa ziara 

 Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Wajumbe wa Menejimenti wakipita kwenye maeneo                                             mbalimbali ya jengo hilo wakati wa ziara 

 Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Wajumbe wa Menejimenti wakipita kwenye maeneo                                             mbalimbali ya jengo hilo wakati wa ziara 
 Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Wajumbe wa Menejimenti wakipita kwenye maeneo                                             mbalimbali ya jengo hilo wakati wa ziara