Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Monday, January 31, 2022

JAJI MKUU AWAALIKA MAJAJI TANZANIA, UINGEREZA KUJADILI ATHARI ZA MFUMO HAKI JINAI

Na Faustine Kapama – Mahakama, Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 31 Januari, 2022 amefungua Kongamano la wadau wa sheria na utoaji haki nchini ambapo amewahimiza washiriki wote kujadili jinsi mfumo wa haki jinai uliopo unavyoathiri wahanga na washitakiwa wa makosa ya jinai.

Amesema kuwa Kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma ni fursa mwafaka kwa Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Uingereza kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali, hususani maeneo ya mfumo wa haki jinai ambapo Mahakama zote mbili wanashiriki changamoto zinazofanana.

"Kwa mfano, hatua ya awali ya shauri la kijinai (committal proceeding) ni eneo ambalo sisi sote tunashiriki. Madhumuni ya msingi ya kuendesha mwenendo huu ni kuamua kama kuna ushahidi wa kutosha kumruhusu mtu anayetuhumiwa kwa kosa kusikilizwa mbele ya Jaji. Kwa nini basi, kuwa na mwenendo huu wenye nia njema ubadilike kuwa kichaka cha ucheleweshaji uliopitiliza nchini Tanzania?” amehoji Mhe. Prof. Juma.

Jaji Mkuu amesema kuwa wamekuwa wakikumbana na ucheleweshaji mkubwa wakati wa kuendesha hatua hizo za awali za mashauri ya jinai yanayosikilizwa na Mahakama Kuu, hivyo katika Kongamano hilo Mtaalamu kutoka Uingereza, Jaji Nic Madge ataweza kutoa uzoefu wake na namna nchi yake inavyofanya ili kuepuka ucheleweshaji huo.

Wawezeshaji wengine katika Kongamano hilo ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, Majaji wengine wabobezi kutoka nchini Uingereza, Jaji Lain Bonomy na Nicholas Blake, Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Awamu Mbangwa, Mhe. Edwin Kakolaki na Mhe. Dkt. Zainab Mango pamoja na Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Bw. Laurean Tibasana.

Jaji Mkuu ana imani kuwa washiriki wa Kongamano hilo watanufaika vya kutosha kutokana na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na  Majaji na wadau wengine ambao wamebobea katika maeneno kadhaa yananyohusu haki jinai. Ametoa shukrani zake kwa Serikali ya Uingereza kwa kuendelea kutoa mchango wa kifedha kupitia mpango endelevu wa kupambana na rushwa (BSAAT).

"Kongamano la leo ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano ulioanza tangu mwaka 2017 katika Mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Jumuiya ya Madola (CMJA). Licha ya janga la UVIKO-19, tunatarajia kuendeleza shughuli mbalimbali, ikiwa pamoja na mafunzo, miaka mingi zaidi ijayo,” Jaji Mkuu amesema.

Awali, akizungumza katika Kongamano hilo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Gerald Ndika, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani amesema kuwa Programu hiyo iliyoandaliwa ni moja ya programu nyingi za maendeleo ya kitaaluma ambazo zimeundwa na Chuo kwa kushirikiana na washirika wake.

Mhe. Dkt. Ndika amesema kuwa Kongamano hilo ni ushuhuda wa wazi kwamba Chuo hicho kimekuwa kikijitahidi kutimiza majukumu yake chini ya Sheria ili kuboresha utoaji wa haki nchini kwa kutoa mafunzo yanayofaa kwa maafisa wa Mahakama na watumishi wengine.

Kongamano hilo limeandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mahakama ya Uingereza na kuratibiwa na Taasisi ya Majaji Wastaafu nchini Uingereza iitwayo Slynn Foundation wakishirikiana na IJA kupitia ufadhili wa Programu ya Kitaifa ya Kuzijengea Uwezo Taasisi za Umma Tanzania zinazohusika na kuzuia na kupambana na Rushwa (BSAAT).

Kuandaliwa kwa Kongamano hilo ambalo litafanyika kwa siku moja ni sehemu ya hitihada za Mahakama ya Tanzania katika kuwajengea uwezo maafisa wa Mahakama na wadau wengine wa sheria ya haki nchini katika kutekeleza majukumu yao hususani utoaji wa haki jinai.

Mbali na maafisa wa Mahakama waliostafu na walioko kazini pamoja na Mahakama ya Uingereza, washiriki wengine katika Kongamano hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na maafisa kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikjali, ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kongamano hilo ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini ambayo kilele chake ni tarehe 2 Februari, 2022, pamoja na mambo mengine, limelenga kujadili uboreshaji mbalimbali uliofikiwa na Mahakama ya Tanzania katika utoaji wa haki jinai pamoja na kubadilishana uzoefu wa namna haki jinai kwa wahanga na washitakiwa unavyofanyika kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Uingereza.

Hii ni mara ya pili Kongamano hili linafanyika baada ya lile la kwanza ambalo lilifanyika katika Wiki ya Sheria mnamo mwezi Februari 2020 jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akihutubia Kongamano linalojumuisha Majaji wa Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Uingereza kujadili, pamoja na mambo mengine, athari za mfumo uliopo wa haki jinai. Kongamano hilo limefanyika leo tarehe 31 Januari, 2022 katika ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.


Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bw. David Concar akisisitiza jambo alipokuwa akiongea kwenye Kongamano hilo.


Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Paul Kihwelo, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani akitoa neno la ukaribisho katika Kongamano linalowaleta pamoja Majaji kutoka Mahakama ya Tanzania na Uingereza.


Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Gerald Ndika akitoa neno la utangulizi katika Kongamano.



Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani (juu) na Mahakama Kuu (chini) waliohudhuria Kongamano hilo.



Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu waliohudhuria kwenye Kongamano.

Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Majaji wa Mahakama Mahakama Kuu ( juu ) na Mahakama ya Rufani (chini) waliohudhuria Kongamano hilo.




Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka Uingereza.



Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu waliohudhuria kwenye Kongamano.

Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka Uingereza.


Meza Kuu, ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Wandamizi wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Msajili Mkuu, Mhe. Wilbert Martin Chuma, Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Kevin Mhina na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Shamillah Sarwatt.


Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani (juu na chini) waliohudhuria Kongamano hilo wakifuatilia mada.




Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania (juu na chini) waliohudhuria Kongamano hilo wakifuatilia mada mojawapo iliyokuwa inawasilishwa na wawezeshaji




Maafisa Wandamizi wa Mahakama ya Tanzania, ambao ni Msajili Mkuu, Mhe. Wilbert Martin Chuma (kushoto) na Mtendaji Mkuu, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kutoka  kushoto) wakiwa na Majaji Wastaafu wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sauda Msafiri na Mhe. Januari Msoffe (kulia) wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zinawasilishwa kwenye Kongamano hilo.

                                 (Picha na Faustine Kapama-Mahakama)

RAIS MWINYI: ZINGATIENI MAADILI NA SHERIA KATIKA UTOAJI HAKI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe, Dkt. Hussein Ali Mwinyi mapema leo amezidua maadhimisho ya Wiki ya Sheria na kuwakumbusha watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau wote wa sekta ya sheria nchini umuhimu wa kuzingatia maadili katika utoaji haki na kuheshimu sheria hatua itakayosaidia kujenga umoja, amani na mshikamano ili kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanatimia.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mhe. Mwinyi amebainisha kuwa kwa nafasi yake kama Rais wa Zanzibar, ambaye ameitumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ngazi mbalimbali ikiwemo uwaziri, anatambua na kuheshimu umuhimu wa sheria kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia anafahamu umuhimu wa sheria katika kujenga umoja, amani, udugu na mshikamano, hivyo mafanikio ya kiuchumi, kibiashara na kiuwekezaji hutegemea kuwepo kwa misingi imara ya utawala bora, sheria na uhuru wa Mahakama.

“Ni dhahiri kuwa ustawi wa wananchi wetu, kwa kiasi kikubwa unategemea kuwepo kwa sheria madhubuti zinazotambua ukweli kuwa wananchi wengi kutoka pande zote mbili za Muungano ni maskini. Hivyo, sheria zetu na taratibu za kimahakama ndizo zitakazosaidia kuwainua na kufanikisha shughuli zao kiuchumi na kijamii, kwa kuwa uwepo wa sheria bora zinazosimamiwa vyema ndio kutafanikisha uchumi wao, biashara na shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato,”amesema Dkt. Mwinyi.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa upo umuhimu wa kuheshimu sheria zetu kwa kuzingatia ukweli kuwa miongoni mwa mambo yanayodhoofisha misingi ya utawala bora ni kuwepo kwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu, uzembe, ikiwa ni pamoja na kukosa uwajibikaji na kutofuata sheria hatua inayopelekea ukiukwaji kwa maadili.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa upo umuhimu wa kuheshimu sheria zetu kwa kuzingatia ukweli kuwa miongoni mwa mambo yanayodhoofisha misingi ya utawala bora ni kuwepo kwa vitendo vya rushwa, ubadhirifu, uzembe, ikiwa ni pamoja na kukosa uwajibikaji na kutofuata sheria hatua inayopelekea ukiukwaji kwa maadili.

“Nachukua fursa hii kupongeza jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Mahakama ya Tanzania katika kuimarisha huduma za kutoa haki kwa wananchi na kuhakikisha mnaongeza kasi ya kusikiliza mashauri mbalimbali yanayowasilishwa katika ngazi zote za Mahakama,” amesema Dkt. Mwinyi.

Rais Mwinyi ameipongeza Mahakama kwa hatua ya kuanzisha Mahakama inayotembea kwani itasaidia kufikisha huduma ya utoaji haki kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini. Huku akipongeza hatua mbalimbali zilizochukuliwa ikiwemo kutafsiri sheria kwa lugha ya Kiswahili, jambo ambalo limewapa Watazania matumaini kama hatua mojawapo ya maendeleo ya sekta ya sheria nchini.

Aidha kiongozi huyo ameshauri kuongeza jitihada za kupata wataalam wa lugha ya alama pamoja na kuimarisha miundombinu inayozingatia uwepo wa Watanzania wenye mahitaji maalum, wakiwemo watu wenye ulemavu wa aina tofauti hatua itakayosaidia makundi maalum kupata haki zao bila kikwazo chochote.

Akizungumzia kuhusu ya ushirikiano iliyopo baina na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mahakama ya Zanzibar. Rais Mwinyi ameelezea kuridhishwa na ushirikiano uliopo huku akiwasihi kuuendeleza ushirikiano huo kwa manufaa mapana ya Taifa.

“Nimeelezwa kuwa uhusiano huo ni wa muda mrefu toka mwaka 1965, nafurahi kuona kuwa ushirikiano huo unaendelezwa kwa kupeana uzoefu na utaalam utakaoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yenu. Natoa wito kuendeleza ushirikiano huo kwa lengo la kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya utendaji na kuongeza kasi na ufanisi katika Mahakama zetu,” alisema.

Mhe. Dkt Mwinyi amepongeza mafanikio makubwa aliyoyaona wakati akitembelea maonesho yaliyoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria, ambapo ameelezwa kuwa huduma zitakazotolewa kwa siku zote za maonesho ni moja ya utekelezaji wa nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa Mahakama na malengo makuu ya nguzo hiyo ni pamoja na kuimarisha imani ya wananchi na kuongeza uelewa na ufahamu wao wa taratibu na shughuli za utoaji haki nchini.

Katika hatua nyingine Rais Mwinyi amekubaliana na uamuzi wa kuzidi kutoa taaluma kuhusu huduma za Mahakama kwani bado haijawafikia wananchi walio wengi. Amebainisha kuwa ni wazi wananchi watanufaika na huduma hiyo, hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kuitumia fursa iliyopo vizuri kwa kufika kwa wingi kwenye maonesho hayo.

“Kupitia maenesho haya pia nimeshuhudia uboreshaji makubwa unaofanywa na unaoendelea kufanywa katika mnyororo mzima wa utoaji haki. Ni dhahiri kuwa uboreshaji mkubwa niliyoshuhudia ya matumizi ya TEHAMA ni dalili njema ya matayarisho makubwa ya kupokea na kuendeleza matumizi ya TEHAMA ndani ya Mahakama zetu. Natoa pongezi za kipekee kwa uongozi wa Mahakama ya Tanzania na watumishi wote kwa kuendeleza uboreshaji huu mkubwa,” amesema.

Mhe. Dkt Mwinyi pia alitumia fursa hiyo adhimu ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria kutoa wito kwa wanasheria na wataalam wote wa sheria, viongozi wa Mahakama na Watumishi wote wa sekta ya sheria kuielewa na kuifanyia kazi mipango mikuu ya uchumi inayotekelezwa na Serikali zote mbili nchini katika jitihada za kupunguza umasikini na kuwa na uchumi unaolingana na ushindani wa karne ya 21, hivyo kuwa huru kutoa ushauri wao wa kisheria kwa lengo la kuifanikisha.

Ameeleza kuwa anatambua kuwa zipo sheria ambazo huenda zikawa ni kikwazo cha kufikia matarajio yetu ya kiuchumi na hasa uchumi wa bluu na ustawi wa jamii, hivyo Sheria hizo zitahitaji kufanyiwa marekebisho ili zifanikishe mipango yetu ya uchumi wa kisasa hivyo naomba tumieni utaalam wenu kuzishauri Serikali zetu kuchukua hatua za kurekebisha sheria ambazo zinakasoro, nasi tutafanya hivyo kwa maslahi mapana ya nchi yetu na Watanzania wote.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yamezinduliwa leo Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali yakiwa na kauli mbiu isemayo Zama za Mapinduzi ya Nne ya Viwanda: Safari ya Maboresho kuelekea Mahakama Mtandao.

Baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na mkewe Mama Mariam Mwinyi wakijiandaa kushiriki matembezi ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma tarehe 23 Januari, 2022.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi (wa tatu kulia) akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipasha viungo kabla ya kuanza matembezi kuadhimisha Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma tarehe 23 Januari, 2022.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wengine wa Serikali katika matembezi kuadhimisha Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma kuanzia tarehe 23 Januari, 2022.


Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi (wa tatu kulia) akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakinyoosha viungo baada ya kukamilisha matembezi ya kilometa saba wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sheria inayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma tarehe 23 Januari, 2022.



Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma tarehe 23 Januari, 2022.


Baadhi ya wadau kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza Mgeni rasmi Dkt. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na yanatarajiwa kukamilika Februari Mosi mwaka huu katika kilele cha Siku ya Mahakama.



Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika banda la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto  katika ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na yanatarajiwa kukamilika Februari Mosi mwaka huu katika kilele cha Siku ya Mahakama.


Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki waliokiwakilsiha Chuo katika maonesho ya  Wiki ya Sheria yaliyoanza Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na yanatarajiwa kukamilika Februari Mosi mwaka huu katika kilele cha Siku ya Mahakama.

Mhe. Gerson John Mdemu , Jaji Mfawidhi  Mahakama Kuu Dodoma na Mjumbe wa Baraza la Uonfozi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akipokea machapisho mbalimbali yaliyotayarishwa na Chuo alipotembelea badha la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwenye maonesho ya  Wiki ya Sheria yaliyoanza Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma 

Baadhi ya wadau wa sheria wakpata elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto  kwenye  maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na yanatarajiwa kukamilika Februari Mosi mwaka huu katika kilele cha Siku ya Mahakama.

Baadhi ya wadau wa sheria wakpata elimu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto  kwenye  maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Januari 23,2022 katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na yanatarajiwa kukamilika Februari Mosi mwaka huu katika kilele cha Siku ya Mahakama.



Tuesday, January 18, 2022

IJA YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAHAKIMU WAKAZI WAPYA

 Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania,  Mhe. Mohamed Chande Othman leo tarehe 18 Januari, 2022 amefungua mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya thelathini na tano. Mafunzo haya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 18 Januari mpaka 22 Januari, 2022. Mahakimu hawa ni wale walioteuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma tarehe 17 Januari, 2022.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Jaji Mkuu Mstaafu aliwaambia Mahakimu hao kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ni ngazi ya uongozi na hivyo wanaingia kwenye mahakama ya mwanzo kama viongozi kwa  mategemeo ya kuongoza watumishi watakaofanya nao kazi  waliochini yao. Pia aliongeza kuwa mahakama inawategemea katika kusimamia mpango mkakati na maboresho ya mahakama ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya Mahakama.

Mhe. Othman aliwasisitiza Mahakimu hao kuwa taswira ya Mahakama ya Mwanzo kwa sasa imebadilika sana na hivyo wao pia waendelee kuibadilisha na kuifanya bora zaidi ili huduma kwa wananchi ziwe bora zaidi na kwa wakati.

 “Mahakama za mwanzo ndio zinatoa fursa kubwa zaidi kwa Watanzania kupata haki kuliko mahakama nyingine zote kwa sababu zimetapakaa Tanzania nzima”, alisema Mhe. Othman.

Hata hivyo Mhe. Othman hakusita kuwakumbusha mahakimu hao kuwa makini kwenye nguzo muhimu ya uhuru wa kila hakimu na uhuru wa mahakama. Aliwasisitiza kuamua mashauri yaliyo mbele yao kwa sheria bila woga wala shinikizo. 

“Watanzania wanataka Mahakama huru, inayotoa haki kwa wakati, mahakama adilifu, Mahakama ambayo ina uwezo na Mahakama ambayo haina gharama kubwa” aliongeza Mhe. Othman.

Mhe. Othman aliwaasa Mahakimu hao kujua na kufuata taratibu zilizowekwa na mahakama wakati wa uendeshaji wa mashauri hadi wanapofikia kutoa maamuzi ikiwemo taratibu za usikilizaji wa shauri na kutoa uamuzi unaoongozwa na sheria pamoja na kuweka sababu za hukumu bila kusahau kupata maoni kutoka kwa wazee wa baraza.

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ni kitovu cha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama  na wadau  wa sheria  nchini.

Mhe. Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kusema mafunzo hayo ni  sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Taifa ya 2013 na Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2021/22-2024/25, Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019 ambayo inaelekeza  kila mtumishi anayeajiriwa, kupanda cheo au kuteuliwa kabla hajaanza majukumu mapya apate mafunzo elekezi kwa lengo la kuboresha huduma za mahakama.

Mhe. Dkt. Kihwelo alielezea Mahakimu hao kuwa Chuo kina Mpango Mkakati wa  miaka mitano wa mwaka 2018/19-2022/23, na eneo ambalo chuo limekuwa likijizatiti ni eneo la mafunzo ya aina hiyo ya kuwajengea uwezo watumishi wa mahakama.

Mhe. Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kuwaomba Mahakimu wajitahidi sana kutoa huduma nzuri na kujiepusha na rushwa kwani kwa sasa mahakama zimeboreshwa kwa kuwa na majengo mazuri sana na hivyo basi huduma ziendane na majengo.

Wakati huohuo,  Mhe. Sharmillah Sarwat, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ameupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa programmu za maboresho yanayaofanyika ikiwepo kuwekeza kwenye  raslimali watu ambapo Chuo  kimekuwa ikifanya kwa vitendo kuwajengea uwezo watumishi hao wa Mahakama wakiwemo Mahakimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na weredi.

1.  Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji, Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akifungua Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.


Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa anawakaribisha washiriki Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto


1. Mhe. Sharmillah Sarwat Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania akitowa utambulisho kwenye Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto


1.   Washiriki wa  Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani) 


1.  Washiriki wa  Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani) 


1.   Washiriki wa  Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani) 

1.    Washiriki wa  Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa wanafuatilia  hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani) 


1.     Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

 

2.    

 

3. 





 Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya Mahakama wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto




    Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya IJA wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

Monday, January 17, 2022

IJA YATOA MAFUNZO YA NAMNA BORA YA USULUHISHI WA MIGOGORO KWA MAAFISA WA EWURA

 Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji, Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania amefungua mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa kumi na tano  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Mafunzo haya ya siku tano yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yanafanyika   kuanzia tarehe 17 Januari mpaka 21 Januari 2022 Chuoni hapo.

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Othman aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo kuwa mafunzo hayo ni fursa kwao kwani watabadilishana uzoefu kwa kuwa mafunzo hayo yamejumuisha washiriki enye taaluma mbalimbali na sio wanasheria peke yake. Aliendelea kwa kusema kwamba kwa hapa nchini usuluhishi katika migogoro mingi haifanywi na wanasheria bali na wanataaluma wengine.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Paul. Kihwelo ameeleza lengo kuu la mafunzo  hayo ni kuwajengea uwezo maafisa hao wa namna ya kusuluhisha migogoro mbalimbali kati ya watoa huduma na wateja. Mkuu wa Chuo aliongeza kwamba mafunzo haya yatasaidia kuongeza ufanisi katika eneo hilo la usuluhishi wa migogoro.

“Tunaamini mafunzo yatasaidia sana kuwajengea uwezo na kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku”. Alisema Mhe. Dkt. Kihwelo.

Aidha, Mhe. Dkt. Kihwelo alieleza kuwa Chuo kina jukumu la kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya sheria ili kuwa na uwezo wa kusuluhisha migogoro mbalimbali inayotokea kwenye Mamlaka au Taasisi mbalimbali na kwa kufanya hivyo itapunguza mlundikano wa mashauri mahakamani.

Wakati huohuo Mjumbe wa Bodi na mshiriki wa mafunzo hayo,  Bw. Fadhili Manongi ameelezea kwamba mafunzo haya yatawasaidia sana katika utoaji wa maamuzi na kuweza kutenda haki pamoja na kutoa ushauri wa nini kifanyike kuhusiana na migogoro watakayokutana nayo.

Bw. Fadhili  ametoa ushauri kwa Mamlaka zote zinazofanya uthibiti, kuja Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kupata mafunzo kama haya.

Mafunzo hayo yamejumuisha maafisa wa EWURA wa ngazi mbalimbali ambao ni Wajumbe wa Bodi na wajumbe wa menejimenti. Mada mbalimbali zitawasilishwa na wawezeshaji mahiri na wabobezi katika masuala ya mbinu za usuluhisi wa migogoro ambao ni Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Robert V. Makaramba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Rose Teemba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.


Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji, Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akifungua mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa    wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani.


Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa anawakaribisha washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa    wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani

Bw. Goodluck Chuwa, Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri  wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akitoa utambulisho kwa washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kwa maafisa    wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) hawapo pichani
Washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia 
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)


Washiriki wa  mafunzo ya Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa wanafuatilia 
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)

Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji na mjumbe wa bodi ya EWURA, kushoto  kwake ni Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Robert V. Makaramba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania(aliyevaa miwani) kulia kwa Mhe. Othman ni Bw. Fadhili Manongi Mjumbe wa Bodi ya EWURA na mwisho kulia ni Mhe. Rose Teemba Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya  Kanuni na Mbinu za Usuluhishi wa Migogoro kutoka  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)