Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Wednesday, December 7, 2022

JAJI MKUU AIPONGEZA IJA KWA KUANDAA VIZURI WAHITIMU WAKE

 Na: Rosena Suka IJA Lushoto

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amekipongeza Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwaandaa wahitimu kwa kuwajengea ujuzi na maarifa katika fani ya sheria kwa ngazi za Stashahada na Astashahada.

 Prof. Ibrahim H. Juma ameyasema hayo kwenye mahafali ya 22 ya Chuo yaliyofanyika Chuoni hapo  leo Desemba, 7 2022. Aidha amesema kuwa wengi wa wahitimu huendelea na ngazi ya juu ya Elimu ya Sheria na huonyesha mafanikio makubwa hii inadhihirisha na  kuthibitisha ubora wa Chuo cha IJA.  Aliendelea kwa kusema  wahitimu wa Chuo wameajiriwa maeneo mbali mbali kama vile Makarani wa Mahakama; Watendaji wa Vijiji/Mitaa; Makatibu Wasaidizi katika Makampuni ya Mawakili; Wasaidizi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania; Makatibu wa Sheria Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mashtaka, Serikali za Mitaa na kadhalika.

Mhe. Prof.  Juma aliendelea kuwasihi wahitimu hao kutumia  elimu waliyoipata kuibadilisha na kuisaidia jamii pale mtakapopata nafasi na uwezo wa kufanya hivyo kwani sheria inahusika na haki.

“Nawaomba mkawe watu wa haki na wenye kiu ya kutenda haki wakati wote katika yote mtakayoyafanya ili jamii ione utofauti wenu na wengine. Kutenda haki hakusubiri tu hadi uwe mtumishi wa Mahakama au mwajiriwa. Ni zoezi endelevu kwa maisha yetu”

Mhe. Prof. Ibrahim H. Juma aliendelea kuwasisitiza wahitimu hao kwa usemi wa kiingereza usemao  “Law is not always the problem. Those who implement the law may be the real problem:” na alifafanua kwa kusema kuwa sio mara zote tatizo huwa ni Sheria au kutokuwepo  kwa sheria nzuri,  bali sheria inaweza kuwa mbaya pale waliopewa dhamana ya kutekeleza sheria ili itimize malengo wanayotarajia kutoka kwa sheria husika.  Aliwaomba wahitimu wa Mahafali hayo  kuwa wasiwe na  tatizo katika utekelezaji wa sheria kwani masomo ya Stashahada ya Sheria na Astashahada ya Sheria waliyopata yamewapa mwanga wa kuelewa Sheria ili  kuweza kutumia sheria kutatua changamoto zitakazojitokeza.   

 Mhe. Prof. Ibrahim Juma aliendelea kwa kuwakumbusha wahitimu kutambua  elimu waliyonayo kuwa haitoshi kwani kasi ya maboresho na Mabadiliko ya Elimu inatakiwa ilingane na Kasi ya Mabadiliko ya Mahitaji ya Jamii.

“Watanzania wa leo wanaishi katika dunia inayosukumwa na Teknolojia yenye nguvu kubwa ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4IR). Wahitimu wenye elimu ya ngazi au daraja lolote ni lazima wahakikishe kuwa elimu waliyopata kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama haitoshi ni lazima waiboreshe kila siku ili ilingane na mahitaji ya ushindani mkubwa katika Karne ya 21”  alisema  Mhe. Prof.  Juma.

 Kwa upande mwingine, Mhe. Prof. Juma amekielekeza Chuo kwamba, katika awamu ya Pili ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (2021-2025), kufanya maboresho ili kiwe Chuo kinachotoa elimu na mafunzo kwa wanafunzi wake na kwa watumishi wa Mahakama kwa kutumia mifumo ya  TEHAMA.  Aliendelea kwa kusema awamu ya Pili ya Maboresho ya Mahakama imetenga jumla ya Dola milioni 6 katika eneo la mafunzo ya kuongeza Ujuzi (Skills) na Maarifa (knowledge).

Aidha, Mhe. Prof. Juma amewasihi Wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Chuo, Wahadhiri, Wakufunzi na watumishi wote wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, kujitayarisha na matumizi ya Jukwaa la Ki-elektroniki kutoa mafunzo na elimu  kwa  waliopo ndani na nje ya Chuo ambapo itaweza kutumika sio tu kwa wanafunzi wa Stashahada na Astashahada ya Sheria, bali pia litatumika kutoa mfunzo  Elekezi na Endelevu kwa Majaji, Wasajili, Naibu Wasajili, Watendaji, Mahakimu na Watumishi wa kada zote.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald A. Ndika  aliwakumbusha wahitimu hao  574 kuwa kuhitimu kwao katika ngazi hizo ni mwanzo  wa safari ndefu ya kitaaluma.  Hivyo ,  na kuwaasa waendelee kutafuta elimu bila kuchoka.

 Mhe. Dkt.  Ndika alieleza kwamba kitaaluma wanachuo wa IJA wamekuwa wakifanya vizuri katika vyuo vya elimu ya juu wanapokwenda kwa ajili ya kuendelea na Masomo yao mara tu wanapohitimu IJA, Hivyo kwa ufanisi huo  inapelekea wanafunzi hao kuajiriwa katika taasisi mbalimbali za utoaji haki nchini kama vile Mahakama. 

 Naye Mkuu wa Chuo na Jaji ya Mahakama  ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo ameeleza kwamba mpaka sasa Chuo kiko mstari wa mbele katika kutoa mafunzo kwa watumishi mbalimbali wa Mahakama kwa njia ya Mtandao, ambapo mafunzo haya yameweza kuwafikia watumishi wa kada ya Mahakimu na Majaji kwenye maeneo mbalimbali ya utendaji kazi.  Kwa njia ya mafunzo imeweza kupunguza gharama kwa Mahakama ya Tanzania.

Mahafali ya 22 ya IJA yameambatana na ufunguzi wa jengo la bweni la wavulana. Bweni hili  lina ghorofa nne na lina uwezo wa kulaza watu 320 na lina thamani ya shilingi za kitanzania billioni 2.6. Ujenzi wa bweni hili ulisimamiwa na Mahakama ya Tanzania katika mpango wa Maboresho ya Mahakama.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa  hotuba wakati wa katika Mahafali ya 22 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) leo tarehe 07 Desemba, 2022.




Wahitimu  wa Astashada ya Sheria wakiwa katika maandano ya sherehe za mahafali zilizofanyika tarehe 07 Desemba, 2022.  chuoni 

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma na meza kuu  katika picha ya pamoja na Jumuiya ya wahitimu wa IJA (IJA ALUMN) 


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma na meza kuu  katika picha ya pamoja na baadhi  Wahitimu wa Stashahada ya Sheria kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Ibrahim Hamis Juma na meza kuu  katika picha ya pamoja na baadhi  Wahitimu wa Astashahada ya Sheria kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akikata utepe  kuashiria uzinduzi wa bweni la wavulana Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). Kushoto ni  Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi  (IJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika,  kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akimkabidhi mfano wa ufunguo   Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi  (IJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Gerald Ndika wakati wa uzinduzi huo.

Tuesday, December 6, 2022

JUMUIYA YA WAHITIMU IJA YAENDESHA KONGAMANO LA KITAALUMA

 Na Rosena Suka, IJA

Mhe. Dkt. Gerald Ndika, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo Desemba 6,  2022  amefungua Kongamano la Kitaaluma lililoandaliwa na Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA ALUMNI) katika ukumbi wa Barnabas Samatta Chuoni Lushoto.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Mhe. Dkt. Ndika alianza kwa kuwapongeza wanajumuiya hao kwa kujitolea na kushiriki katika shughuli mbalimbali zenye nia ya kutoa elimu na kukuza uelewa katika jamii kuhusiana na masuala ya sheria ikiwepo kuandaa makongomano ya kitaaluma kama hilo, kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi bure na kushiriki katika masuala mbalimbali yanayoandaliwa na Chuo kwa lengo la kuwaunganisha na kuwajengea umoja wahitimu wote wa chuo.  

Mhe. Dkt. Ndika aliendelea kwa kusema kongamano hilo ni fursa nzuri kwa washiriki kudadavua masuala muhimu yahusuyo mambo mbalimbali ya kiuchumi na ya kijamii, sambamba na kuangalia ukuaji katika maeneo ya utoaji haki.

 “ Na ni mategemeo ya Chuo na Taifa kwa ujumla kwamba kila mmoja wenu mara baada ya kuhitimu kwenu mnapaswa kuelewa kwamba nafasi nliyonayo ni vema mkaitumia katika kuleta maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla ili kukuza taaluma na kuielimisha jamii katika utoaji haki, mkizingatia usawa, Amani na usalama” alisema Mhe. Dkt. Ndika.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akiwa anafunga kongamano hilo aliwahimiza washiriki wa kongamano  kutumia fursa hiyo ili kuwa na mahusiano mazuri na kuitumia Jumuiya ya Wahitimu hao ili kupata fursa mbalimbali za kujifunza katika taaluma waliyonayo.

Kongamano hilo lililowashirikisha wanachuo wote lililoongozwa na mada isemayo “IJA and Prospects for offering practical legal training to lawyers Employed in Public Service ; Practicalities and Challenges” na hufanyika mara moja kila mwaka siku moja kabla ya sherehe za mahafali ya Chuo.

Mkuu wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akiwa katika picha ya pamoja na Jumuiya ya Wahitimu wa IJA  baada kufungwa kwa kongamano hilo.




Picha mbalimbali za washiriki wakiwa wanafuatilia Kongamano