Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Tuesday, February 22, 2022

IJA YAWANOA MAHAKIMU 36 UENDESHAJI MASHAURI KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA

 Na: Rosena Suka, Lushoto

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kimeandaa na kuendesha mafunzo kuwajengea uwezo Mahakimu 36 namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na chuo hicho kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) kupitia ufadhili wa USAID kutoka kwa watu wa Marekani  yamefunguliwa na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tanga, Mhe. Latifa Mansoor, tarehe 22 Februari, 2022 na  yanahusisha Mahakimu Mahakimu wa ngazi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mbeya, Njombe na Kilimanjaro.

Akizungumza na washiriki wakati wa ufunguzi, Mhe. Mansoor amewafahamisha lengo la  mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi wa kutekeleza majukumu ya namna bora ya kuendesha kesi za ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia manusuru wa ukatili huo na kuhakikisha wanapata haki na watuhumiwa kushughulikiwa  kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Mhe. Mansoor amefafanua kuwa ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa ambalo linaikabili Dunia kwa kuonesha tatifiti mbalimbali zinazotolewa na mashirika mengi yaliyofanya tafiti hizo. Tafiti iliyofanywa na Shirika la Afya Duniani mwaka 2013 zimeonyesha asilimia 35 ya wanawake Duniani wamefanyiwa ukatili wa kupigwa au kubakwa. 

Amenainisha kuwa katika tafiti iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) ya mwaka 2017 imeonesha wasichana wapatao 750 milioni duniani wanaolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.  Kwenye taarifa hiyo imekadiria kuwa wasichana milioni 120, yaani msichana moja katika ya kumi Duniani, wamekumbana na vitendo vya kulazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao.

Aidha, Mhe. Mansoor alieleza kuwa rushwa ya ngono ni tatizo lililopo katika maeneo ya kazi na vyuo vikuu nchini kutokana na utafiki uliofanywa na TAKUKURU katika vyuo viwili nchini mwaka 2020 na  asilimia 50 ya waliohojiwa walikiri rushwa hii kuwepo katika vyuo vikuu.

Mhe. Mansoor amezitaja hatua mbalimbali za Serikali katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia hapa nchini, ikiwemo kuanzisha Madawati ya Jinsia na Watoto katika vituo vya Polisi, kwa lengo la kuhakikisha wanawake na umma kwa ujumla wanakuwa na mazingira mazuri bila vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Pia kuweka wataalamu mbalimbali kwenye vituo vya Mkono kwa Mkono vya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ambao ni wataalamu wa ustawi wa jamii, wanasheria, madaktari na polisi.

Kumekuwepo na huduma za simu bila malipo kwa watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji (Child Helpline), kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika ngazi zote kuanzia kitaifa mpaka chini  na hatua nyingine nyingi.

Mhe. Mansoor amewasisitiza Mahakimu hao kuwa pamoja na juhudi mbalimbali za Serikali za kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia haziwezi kuzaa matunda iwapo hazitaungwa mkono na wadau muhimu kama Mahakama hususani Mahakimu. 

“Katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia, inabidi Mahakama ijikite katika kubuni mikakati ya kisheria ambayo ndiyo italeta suluhisho la kudumu katika kusikiliza kesi za ukatili na kuzitolea maamuzi,” alisema.

Mhe. Mansoor ameainisha kuwa katika utekelezaji wa sera na sheria kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu inayoainisha makosa ya ukatili wa kijinsia kipengele cha (SOSPA) ni mojawapo ya eneo linaohitaji kusimamiwa kikamilifu na Mahakama ili kulinda ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Ni dhahiri kuwa kwa kuwekeza katika sekta ya Mahakama itasaidia kupunguza na kuondoa kabisa vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vina kwambisha juhusi za maendeleo ya nchi” alisema Mhe. Mansoor.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika, Dkt. Monica Mhoja amesema kuwa shirika hilo  linatumia sheria kama nyenzo ya kuleta mabadiliko. 

Amesema Shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ambao ni Wizara ya Katiba na Sheria, Mahakama, Polisi, Kamati za MTAKUWWA, Ofisi ya Bunge, Taasisi za elimu ya juu na kati, Shule za Msingi na Sekondari,  Viongozi wa Dini, Wana Habari, Makundi Maalumu kama watu wenye ulemavu na mashirika mengine. 

Dkt. Mhoja aliendelea kusema kuwa mchango wa WiLDAF katika mabadiliko ya sheria kandamizi na mila na desturi kandamizi ( sheria ya umiliki wa ardhi, sheria ya mirathi, sheria ya ndoa) ni kutoa  msaada wa kisheria na nafasi yao kama afisa wa Mahakama katika kuwahudumia manusura wa ukatili wa kijinsia.

Amesema pia kuwa hutoa mafunzo na kusimamia wasaidizi wa kisheria.  Kwa kupitia mradi wa Mwanamke Imara WiLDAF imepata fursa ya kuaandaa mafunzo kwa Mahakimu katika mikoa ya Njombe, Mbeya na Kilimanjaro ili kuimarisha uwezo wao katika kuhudumia manusura wa ukatili wa kijinsia.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tanga, Mhe. Latifa Mansoor akiongea na Mahakimu wa ngazi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mbeya, Njombe na Kilimanjaro wanaohudhuria mafunzo ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika, Dkt. Monica Mhoja akiongea na Mahakimu wa ngazi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mbeya, Njombe na Kilimanjaro wanaohudhuria mafunzo ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto


Hakimu Mkazi Mfawidhi (W) Lushoto, Mhe. Rose Ngoka akitoa neno la ukaribisho kwa Mahakimu wa ngazi mbalimbali kutoka Mikoa ya Mbeya, Njombe na Kilimanjaro wanaohudhuria mafunzo ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto


Mahakimu wa ngazi mbalimbali na washiriki wa mafunzo  ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto wakiwa wanafuatilia mada zinazotolewa kwenye mafunzo.


Mahakimu wa ngazi mbalimbali na washiriki wa mafunzo  ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto wakiwa wanafuatilia mada zinazotolewa kwenye mafunzo.
Mahakimu wa ngazi mbalimbali na washiriki wa mafunzo  ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto wakiwa wanafuatilia mada zinazotolewa kwenye mafunzo.


Mahakimu wa ngazi mbalimbali na washiriki wa mafunzo  ya kujengewa uwezo wa  namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kuwahudumia wahanga na mashahidi yanayofanyika Chuoni Lushoto wakiwa wanafuatilia mada zinazotolewa kwenye mafunzo.

Saturday, February 12, 2022

MAHAKIMU WAKAZI WATAKIWA KUWAJIBIKA KWA UMMA KWA MUJIBU WA KIAPO: MHE. MSAJILI GODFREY ISAYA

 Na. Rosena S. Suka IJA

Naibu Msajili na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, amewataka Mahakimu Wakazi   kuwajibika kwa umma kwa mujibu wa kiapo walichoapa cha uhakimu ambacho ni kutenda haki kwa wote bila kujali ni nani aliye mbele yake.

Hayo yalisemwa na  Mhe. Godfrey Isaya  leo tarehe 12 Februari, 2022 alipokuwa akifunga mafunzo kwa kundi la tatu na Mahakimu Wakazi sitini na moja kati ya Mahakimu Wakazi 200 ambao wamehudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA) 

Aliongeza kuwa hivi sasa Tanzania iko katika Mapinduzi ya Nne ya Viwanda,  hivyo amewasisitiza washiriki hao kuwa waadilifu na wenye uelewa wa kutosha wa sheria, miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali zitakazowaongoza katika utendaji wao wa kazi za kila siku.  

“Ni wajibu wetu kufanya kazi ya uhakimu kwa uweledi, umakini, uadilifu na kwa kuzingatia ushahidi, miongozo mbalimbali. Nje ya hapo ni kukiuka kiapo cha uhakimu. Ninatambua wazi mnafahamu jambo hili lakini niwaombe mwendelee kusimama kwenye mstari sahihi”. Alisema Mhe. Godfrey.

Mhe. Godfrey aliwakumbusha Mahakimu hao kuwa mafunzo waliyopata yana maana kubwa kwao sio tu  kuwapa nyenzo za namna ya kukabiliana na mashauri ya aina hiyo bali pia watakapoendesha mashauri hayo inavyostahiki watakuwa wametimiza nguzo ya Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania ya kuongeza imani ya wananchi kwa mahakama ambapo itaweza kudumisha amani, utulivu na udugu na kuifanya serikali  kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi.

Naye Mratibu wa Mafunzo na Hakimu Mkazi Mwandamizi  kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto , Mhe. Victor Bigambo amewataka mahakimu hao kuwa walimu kwa wenzao ambao wamebaki vituoni kutokana na ufinyu wa bajeti ambapo umefanya mahakimu hao wachache kuhudhuria kwenye mafunzo hayo, huku akisisitiza kuzingatia masuala ya TEHAMA  ili a kumaliza mashauri yote kwa haraka na kwa ubora kama ambavyo wanapaswa kufanya.

Akizungumza wakati wa kutoa neno la shukurani, Hakimu Mkazi, Bittony I Mwakisu kwa niaba ya washiriki wenzake alisema wanaishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na BSAAT  kuratibu Mafunzo hayo, ambayo yatawasaidia  katika utatuzi wa kesi zinazohusu namna bora ya kuendesha mashauri ya rushwa, utakatishaji fedha na urejeshaji wa mali iliyopatikana na fedha haramu.

Mafunzo haya yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Mradi wa Kujengea Uwezo Endelevu Taasisi za Umma zinazohusika na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Buildingi Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania) BSAAT.

Mafunzo hayo yamehuhusisha  jumla ya Mahakimu wakazi 200 kutoka katika mahakama mbalimbali za Tanzania Bara kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza yenye Mahakimu 61 walimaliza mafunzo tarehe 8 Februari, 2022.  Awamu ya pili ya mafunzo haya yenye jumla ya Mahakakumu Wakazi 69 ilimalizika tarehe 10 Feburari, 2022 na awamu ya tatu naya mwisho iliyojumuisha jumla ya Mahakimu Wakazi 61 imemalizika leo tarehe 12 Februari, 2022.



Naibu Msajili na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya akiwa akitoa hotuba yake kwa kundi la tatu la Mahakimu Wakazi kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA) 

Hakimu Mkazi Mwandamizi na Mratibu wa Mafunzo Mhe. Victor Bigambo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA)  akiongea na washiriki wa mafunzo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali  



Hakimu Mkazi  na mwakilishi wa washiri wa Mafunzo Mhe. Bittony I Mwakisu akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali wakati wa kufunga mafunzo hayo





Baadhi ya  washiriki wa  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali wakipokea vyeti vya ushiriki wa mafunzo wakati wa kufunga mafunzo hayo

(Picha na Ibrahim Mdachi)

Wednesday, February 9, 2022

UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU: MHE. DKT. ZAINABU MANGO

 Na: Rosena Suka IJA  Lushoto 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Zainabu Mango amewataka Mahakimu kushirikiana ili kuendeleza jukumu kuu la Mahakama la kutoa haki kwa wakati kwani umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

 Mhe. Dkt. Mango ameyasema hayo leo tarehe 8 Februari, 2022 alipokuwa anafunga mafunzo kwa kundi la kwanza la Mahakimu Wakazi sitini na moja kati ya Mahakimu Wakazi 200 wanaohudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA)

Katika hotuba yake, Mhe. Dkt. Mango alitoa pongezi kwa uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuweza kuratibu mafunzo hayo chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Mhe. Dkt. Mango aliwasisitiza washiriki hao kuwa wananchi wengi ni wahanga wa makosa ya rushwa na utakatishaji fedha hivyo wanapoamua kesi hizo wanapaswa kutambua maendeleo na ustawi wa nchi yetu na maisha ya mmoja mmoja yako hatarini kutokana na vitendo hivyo.

Jaji Mango aliendelea kuwaomba washiriki hao kutumia uhuru walionao kuamua mashauri ya aina hii bila kuonea mtu kwa hisia au  pasipo na Ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani

“Hii ni kanuni mojawapo ya utoaji haki na ni imani yangu mtaendelea kuitumia ipasavyo” alisema Mhe. Dkt. Mango.

Aidha, aliwapongeza washiriki hao kwa utulivu wao wakati wote wa mafunzo na kuwataka kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyofundishwa na kuendelea kujifunza zaidi mambo mengine ambayo hayakufundishwa ili wawe na uelewa wa kutosha na kuboresha utendaji  wenye ufanisi kwa maslahi mapana ya taifa letu na mahakama kwa ujumla.

Mhe. Dkt. Mango  aliendelea kwa kuwakumbusha washiriki hao kuwa ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa Mahakama na kuzitimiza nguzo zake zote tatu lazima kuzingatia C tatu ambazo ni consultation, coordination na cooperation.

“Hapa nisisitize nyote kuwa na ushirikiano kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Heshima na upendo pamoja na mapenzi mema ya taifa letu yawe ni mambo ya msukumo yatakayotufanya tusimame kwa pamoja ili Mahakama iweze kutekeleza vema jukumu lake la utoaji haki kwa wakati. Mabadiliko na maboresho tunayoyataka hayawezi kufikiwa kwa kiwango tunachokusudia kama hatutakuwa kitu kimoja” alikumbusha Mhe. Dkt. Mango.

Akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki Hakimu Mkazi,  Mhe. Respicius R. Katabi, ameupongeza uongozi mzima wa Mahakama na Mradi wa BSAAT kwa kuandaa mafunzo hayo ambapo wameweza kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo mashauri ya rushwa na kutakatisha fedha hususani uchukuaji ushahidi kwa kutumia TEHAMA.  Ameahidi elimu waliyoipata wataifikisha kwa watumishi wengine wa kada yao ambao hawakuweza kuhudhuria mafunzo hayo.

Mafunzo haya yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Mradi wa Kujengea Uwezo Endelevu Taasisi za Umma zinazohusika na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Buildingi Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania) BSAAT.

Jumla ya Mahakimu Wakazi 200 kutoka katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania wanatarajiwa kupata mafunzo haya katika awamu tatu ambapo awamu ya kwanza yenye Mahakimu 61 wamemaliza mafunzo tarehe 8 Februari, 2022.  Awamu ya pili ya mafunzo haya itaanza tarehe 9 – 10 Feburari, 2022 na awamu ya tatu naya mwisho itakuwa tarehe 11-12 Februari, 2022.



Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Zainab Mango akitoa hotuba ya kufunga mafunzo kwa kundi la kwanza la Mahakimu Wakazi sitini na moja kati ya Mahakimu Wakazi 200 wanaohudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA)



Hakimu Mkazi, Mhe. Respicius R. Katabi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa  mafunzo kwa kundi la kwanza la Mahakimu Wakazi sitini na moja kati ya Mahakimu Wakazi 200 wanaohudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA)


Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania, Mhe. Awamu Mbagwa akiwasilisha mada  kwa kundi la kwanza la Mahakimu Wakazi sitini na moja kati ya Mahakimu Wakazi 200 wanaohudhuria  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA)



 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA) wakipokea vyeti vya ushiriki baada ya kuhudhuria siku mbili za mafunzo.



 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya  mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali yanayoendeshwa na  Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. (IJA) wakipokea vyeti vya ushiriki baada ya kuhudhuria siku mbili za mafunzo.

(Picha na Ibrahimu Mdachi IJA)

Monday, February 7, 2022

CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO CHAENDESHA MAFUNZO KWA MAHAKIMU WAKAZI 200

 Na Rosena Suka –Lushoto

Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kinaendesha mafunzo kwa Mahakimu Wakazi 200 ili kuwajengea uwezo katika masuala mbalimbali ya haki jinai, hususani uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali.

Akifingua mafunzo leo tarehe 7 Februari, 2022, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Edwin Kakolaki amesema anafahamu kuwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Kitengo cha mafunzo cha Mahakama ya Tanzania wameendelea kushirikiana katika eneo la mafunzo.

“Ushirikiano huu ni sehemu tu ya jitihada zinazoendelea katika utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya mwaka 2019 ambayo inatambua Chuo hiki kama kitovu cha utoaji wa mafunzo kwa watumishi wa Mahakama kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji wa Mahakama ya Tanzania,” amesema.

Kwa mujibu wa Jaji Kakolaki, mafunzo hayo kwa Mahakimu hao ni muhimu sana kwao kwani yatawaongezea mbinu na uelewa juu ya masuala mbalimbali ambayo yatawasaidia katika utendaji wa kazi, hivyo amewaomba kushirikiana na wawezeshaji wote katika kupata yale yaliyokusudiwa.

Jaji Kakolaki amebainisha kuwa kesi za rushwa na utakatishaji fedha zipo katika maeneo mengi ikiwemo uchumi na elimu, hivyo Mahakimu Wakazi hawana budi kuwa na uelewa, maarifa na uwezo wa kukabiliana nazo, hasa kwenye suala la kusikiliza na kufikia uamuzi.

“Miongoni mwa madhara yanayoweza kusababishwa na rushwa pamoja na utakatishaji fedha ni kuzuia ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa zima kwa ujumla. Kwa kuzingatia uwepo wa vitendo vya rushwa na utakatishaji fedha katika Idara na Taasisi mbalimbali za Umma na binafsi, serikali imeweka mfumo wa kuzuia na kupambana na vitendo hivyo ili kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinafikia malengo ya kuwahudumia Watanzania kwa haki na usawa,” amesema.

Jaji Kakolaki anamshukuru Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa kutoa kibali cha kufanyika kwa mafunzo hayo yatakayowapatia Mahakimu waliotoka sehemu mbalimbali hapa nchini elimu na ujuzi stahiki katika maeneo ya utekelezaji wa majukumu yao pamoja na mahusiano sahihi kiutendaji kati yao na wadau wengine ndani na nje ya Mahakama.

Aidha, ameishukuru serikali kupitia Programu ya Kitaifa ya Kuzijengea Uwezo Taasisi za Umma Zinazohusika na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (BSAAT) kwa kudhamini mafunzo hayo ya Mahakimu wakazi 200. Amesema kuwa programu hiyo imekuwa msaada mkubwa katika kuwajengea uwezo Mahakimu kupitia mafunzo yahusuyo Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania.

Jaji Kakolaki pia ameushukuru Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) chini ya Mhe. Dkt. Paul Kiwhelo, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Kitengo cha Mafunzo cha Mahakama ya Tanzania chini ya Bi. Patricia Ngungulu kwa kushirikiana kwa ukaribu kuratibu uandaaji wa mafunzo hayo kwa ufanisi mkubwa.

Akitoa neno la utangulizi katika mafunzo hayo, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Martin Chuma aliwakumbusha Mahakamu hao kuwa kazi ya kutoa haki ni kazi ya Mungu na kwa kuwa yeye ni mtakatifu ni lazima kuifanya kwa uadilifu na utakatifu wake.

“Hoja hii ndiyo imelazimu uongozi wa Mahakama kutoa kibali ili mafunzo haya yafanyike. Kwa msingi huo, kupambana na rushwa, utakatishaji fedha na uhujumu uchumi kwa ujumla, si tu unataka weledi wa hali ya juu, lakini pia unahitaji ujuzi na uelewa wa kutosha wa sheria na kanuni zinazohusika na masuala haya,” amesema.

Kwa mujibu wa Mhe. Chuma, rushwa, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ni hatarishi kwenye jamii pamoja na maendeleo ya taifa kwa ujumla, hivyo washiriki hawana budi kusikiliza kwa makini na kushiriki kikamilifu wakati wote wa mafunzo ili kuungana na jitihada zinazoendelea za Mahakama ya Tanzania za kujenga imani na kuwa karibu zaidi na wananchi.

“Ni dhahiri kwamba kila mmoja wetu akiwa na utamaduni wa uadilifu, uchumi wetu utakua, sekta ya umma itakuwa bora na kustawi na taasisi zetu zitaaminika zaidi. Vilevile jamii zetu zitafaidi matokeo ya ukuaji wa uchumi. Zaidi, ustawi wa watu wetu unategemea sana uadilifu wetu na wa viongozi wenzetu. Kwa ufupi uadilifu utaboresha maisha ya watu,” amesema.

Awali, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Stephen Magoha aliwapitisha washiriki wa mafunzo hayo katika maelezo mafupi juu ya   Programu ya BSAAT ambayo imejikita katika kujenga mfumo endelevu wa mapambano dhidi ya rushwa unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Ofisi ya “Foreign Commonwealth Development (FCDO)” kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya na hapa nchini kuratibiwa na Ofisi ya Rais, IKULU.

“Programu hii ni ya miaka mitano na imeanza kutekelezwa mwaka 2018/2019 – 2022/2023 kwa kunufaisha taasisi na wizara mbalimbali, ambapo Mahakama ya Tanzania wakiwa ni moja wapo. Programu hii inatekeleza malengo yake makuu, ikiwemo kupunguza vitendo vya rushwa kama kikwazo cha kupunguza kiwango cha umasikini kwa Watanzania, kuboresha uadilifu, kuboresha uwezo na uratibu wa mfumo wa haki ya jinai katika vita dhidi ya vitendo vya rushwa na kuongeza imani kwa umma juu ya utendaji kazi wa Mahakama,” amesema.

Kwa mujibu wa Bw. Magoha, tangu program hiyo ianze kutekelezwa, kumekuwa na viashiria mbalimbali vya mafanikio ambavyo vimeonekana katika maeneo mbalimbali kama kuongezeka kwa utoaji wa taarifa za ubadhirifu au vitendo vya rushwa kwenye mamlaka husika, kupunguza muda wa usikilizwaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji wa mali.

Wakati wote wa mafunzo, washiriki watapitishwa katika mada mbambali zilizoandaliwa na Wawezeshari mahiri katika maeneo juu ya Rushwa, Utakatishaji Fedha na Urejeshaji Mali. Wawezeshaji hao ni pamoja na Mhe. Kakolaki na Majaji wengine wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt Zainab Mango na Mhe. Awamu Mbagwa pamoja na Naibu Msajili, Mhe. Godfrey Isaya, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mafunzo haya yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania na kuendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto chini ya ufadhili wa Mradi wa Kujengea Uwezo Endelevu Taasisi za Umma zinazohusika na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Buildingi Sustainable Anti-Corruption Action in Tanzania) BSAAT. Jumla ya Mahakimu Wakazi 200 kutoka katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania wanategemewa kupewa mafunzo haya katika awamu tatu ambapo awamu ya kwanza yenye Mahakimu 61 wameanza mafunzo tarehe 7 – 8 Februari, 2022.  Awamu ya pili ya mafunzo haya itaanza tarehe 9 – 10 Feburari, 2022 na awamu ya tatu naya mwisho itakuwa tarehe 11-12 Februari, 2022.






    Mhe. Edwin Kakolaki, Jaji wa Mahakama Kuu Ya Tanzania akifungua Mafunzo kwa Mahakimu Wakazi kuhusu Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.



Mhe.  Victor Bigambo Hakimu Mkazi na Mratibu wa Mafunzo ya kuhusu Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu  akiwatambulisha washiriki kwenye mafunzo yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.



Bw. Stephen Magoha,  Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Mratibu wa BSAAT katika Mahakama ya Tanzania akiwakaribisha washiriki wa mafunzo ya namna bora ya Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.

Picha za washiriki wa mafunzo ya namna bora ya Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu wakifuatialia hotuba ya mgeni rasmi alipokuwa anafungua mafunzo hayo yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.


Picha za washiriki wa mafunzo ya namna bora ya Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu wakifuatialia hotuba ya mgeni rasmi alipokuwa anafungua mafunzo hayo yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.


Baadhin ya picha za washiriki wa mafunzo ya namna bora ya Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu wakifuatialia hotuba ya mgeni rasmi alipokuwa anafungua mafunzo hayo yanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.


Mhe. Edwin Kakolaki, Jaji wa Mahakama Kuu Ya Tanzania na Mwezeshaji wa Mafunzo Namna Bora ya  Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu akiwasilisha mada katika mafunzo hayoyanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.

Mhe. Dkt Zainabu Mango, Jaji wa mahakama kuu Tanzania kanda ya Dar es salaam na mwezeshaji wa mafunzo Namna Bora ya  Uendeshaji Wa Mashauri Ya Rushwa, Utakatishaji Fedha Na Urejeshaji Mali zilizopatikana kwa Fedha Haramu akiwasilisha mada katika mafunzo hayoyanayofanyika Chuo Cha Uongozi Wa Mahakama Lushoto (IJA) Kuanzia Tarehe 7- 12 Februari, 2022.