Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma

Jaji kiongozi wa Tanzania

Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania (katikakati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa stashahada ya sheria

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Mahafali ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yaliyofanyia 18 Desemba, 2020

Friday, July 30, 2021

KUFUNGULIWA DIRISHA LA UDAHILI WA NAFASI ZA MASOMO KWA MWAKA 2021/2022

Monday, July 26, 2021

MAFUNZO YA KUJIANDAA KUSTAAFU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo amefungua rasmi mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwa Watumishi wapatao 84 wa Mahakama ya Tanzania kutoka kwenye kanda mbalimbali za Mahakama ya Tanzania. Mafunzo haya yanafanyika katika ukumbi wa Magadu uliopo mkoani Morogoro kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 26 mpaka 30 Julai, 2021. Bwana Nkembo, alipokuwa akifungua mafunzo hayo aliwapongeza washiriki hao kwa kuwa watumishi bora kwa muda wote waliotumikia Mahakama ya Tanzania mpaka utumishi wao unapokoma. 
Pia aliendelea kwa kuwasisitiza washiriki hao kuwa makini na wizi wa mitandaoni na kwamba utapeli na rushwa ni matukio mabaya ambayo wastaafu wengi wamekutana nayo na kuwataka kuchukua tahadhari zote za kukabiliana nayo. Kwa upande wake, Mtendaji wa Mahakama ya Tanzania, mkoa wa Morogoro ndugu Nestory Mujunangoma amewataka washiriki hao kufanya maandalizi ya kustaafu mapema na kuchukua maamuzi sahihi ambayo hayataathiri maisha yao baada ya kustaafu huku akilinganisha kustaafu kama kubadili gia kwenye gari na kwamba maisha yanaendelea hata baada ya kustaafu kama ambavyo gari huendelea hata baada ya kubadili gia.

Naye Mratibu wa Mafunzo hayo Ndugu Nuhu Mtekele, Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto aliewaeleza washiriki hao kuwa mafunzo hayo ni mpango wa utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2013, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019 pamoja Mpango Mkakati wa Chuo wa miaka mitano wa mwaka 2018/19-2022/23. 

Ndugu Mtekele aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na mafunzo ya darasani, washiriki watapata fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro ili kujionea kwa vitendo miradi na shughuli za ujasiriamali na uwekezaji katika nyanja za kilimo na ufugaji na zile ambazo wanaweza kupenda kuzifanya na hatimaye kuwasaidia kimaendeleo baada ya kustaafu.

Mafunzo hayo yameratibiwa na kuendeshwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Mafunzo hayo yamejumuisha washiriki wa kada mbalimbali wakiwepo mahakimu, wasaidizi wa kumbukumbu, makatibu mahususi, walinzi n.k.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo akifungua rasmi mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwa Watumishi wa Mahakama ya Tanzania ambao hawapo pichani
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kustaafu.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kustaafu.
Picha mbalimbali za washiriki wa Mafunzo ya Kujiandaa kustaafu wakiwa wanafualitia ufunguzi wa mafunzo hayo ulifanyika katika ukumbi wa Magadu Mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na sekreatieti.

Tuesday, July 20, 2021

UZINDUZI WA KITABU CHA MKUSANYIKO WA MASHAURI YA MTOTO (COMPENDIUM OF CHILD JUSTICE CASES) NA RIPOTI YA TATHMINI YA MAFUNZO YA UENDESHAJI WA MASHAURI YA MTOTO (REPORT ON THE IMPACT ASSESSMENT OF TRAININGS TO JUVENILE JUSTICE FRONTLINE WORKERS)


Jaji mkuu wa Tanzania. Mhe. Prof. Juma ametoa pongezi hizo kwenye uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2021. Kitabu hicho kilichoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania kupitia ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya mtoto (UNICEF). Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, 

Mhe. Prof. Juma amezitaka mamlaka zinazosimamia na kutetea haki za mtoto kufanya kazi kwa kushikiana pamoja na kushiriki katika mafunzo mbalimbali yanayohusu mada za uendeshaji ya mashauri ya mtoto ili kuweza kuboresha mfumo wa ufatiliaji madai ya haki za mtoto kwa kushirikiana na mahakama nchini. Mhe. Jaji Prof. Juma aliendelea kwa kusema kuwa wadau wa haki ya mtoto wanapaswa kushilikiana katika kutoa kipaumbele kwa masilahi ya haki za mtoto. 

Mhe. Prof. Juma amesema kuwa haki ya ulinzi pamoja na ustawi wa mtoto hauwezi kupatikana kwa kuiachia chombo cha mahakama peke yake bali inapatikana katika mfumo jumuishi wa haki ya mtoto ambao ni kivuli katika kuhakikisha usitawi na maendeleo ya mtoto, Kwa upande mwingine, Mhe. Jaji Prof. Juma alitoa wito kwa Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa kanda zote nchini, Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa na Mahakama za Wilaya kuhakikisha kuwa wanapata nakala za kitabu hicho katika ofisi zao kwa ajili ya matumizi yao ili kusaidia kufanya rejea inapotakiwa kufanya hivyo. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Dkt. Paul Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani amesema kwa kushirikiana na Mahakama kuu ya Tanzania chini ya ufadhili wa Shirika la kuhudumia watoto dunia UNICEF uongozi wa chuo umekuwa ukiendesha mafunzo mbalimbali yanayohusu namna bora ya usimamizi wa kesi za mtoto mahakamani. 

Akitaja faida kadhaa za kitabu hicho, Mhe. Jaji Mkuu alisema kuwa kitabu hiki kinakumbusha kuwa, zipo sheria nyingi zaidi ya Sheria ya Mtoto ya 2009 [Law of the Child Act Na. 21 ya 2009], na kuwa Haki Mtoto haipatikani ndani ya Sheria moja tu bali kuna vifungu vya Katiba, Sheria mbalimbali, Kanuni, Taratibu, Mazoea na vigezo vingi ambazo kwa pamoja vinaleta mtirirko wa kufahamu mapana na marefu ya Haki ya Mtoto. 

Naye Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto amesema kuwa Chuo  kimekuwa kikifanya tathimini katika kanda zote za mahakama kuu ili kuhakisha wadau mbalimbali walioshiriki kwenye mafunzo ya haki za mtoto wanaendelea kuwa na uelewa mkubwa katika kujuwa namna ya kusimamia kesi za madai kwa watoto mahakamani. 

Mhe. Dkt Kihwelo aliendelea kwa kusema kuwa, hata hivyo kitabu cha mkusanyiko wa kesi za watoto kimetayarishwa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa maamuzi mengi ya mahakama za juu kuhusu haki za watoto kwa maafisa wa mahakama pamoja wadau wa wengine wa haki za mtoto ili kuweza kuongeza uelewa wa maamuzi mbalimbali yanayohusu haki ya mtoto mahakamani kupitia sheria ya mtoto ya mwaka 2009. 

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaohudumia Watoto (UNICEF), Bi. Sampathi Perera alitoa pongezi nyingi kwa Mahakama ya Tanzania na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kufanikiwa kuzindua kitabu hicho na kueleza kwamba uzinduzi wa kitabu hiki mafanikio makubwa sana kwani itawawezesha Majaji na Mahakimu kuendelea kutoa maamuzi sahihi kuhusu mashauri ya Watoto. 

 Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) 2018/2019-2022/2023 wa kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya sheria nchini. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya Sheria nchini wanaohusika na haki za mtoto wakiwemo Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu wa ngazi mbalimbali, Wawakilishi wa Taasisi za Serikali, Wawakilishi kutoka Mashirika yasiyo ya Serikali na Wawakilishi wa UNICEF.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akizungumza na wadau wa Sheria wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha Mkusanyiko wa Mashauri ya Watoto (Compendium of Child Justice Cases) pamoja ripoti ya tathimini ya mafunzo kwa wadau wa haki za watoto (report on the impact assessment of trainings to juvenile justice frontline workers) . 



Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaohudumia Watoto (UNICEF), Bi. Sampathi Perera akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha Mkusanyiko wa Mashauri ya Watoto (Compendium of Child Justice Cases) pamoja ripoti ya tathimini ya mafunzo kwa wadau wa haki za watoto (report on the impact assessment of trainings to juvenile justice frontline workers)

Wadau wa sheria kutoka katika vyombo mbalimbali vya sherria wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Mkusanyiko wa Mashauri ya Watoto (Compendium of Child Justice Cases) pamoja ripoti ya tathimini ya mafunzo kwa wadau wa haki za watoto (report on the impact assessment of trainings to juvenile justice frontline workers)