Pia aliendelea kwa kuwasisitiza washiriki hao kuwa makini na wizi wa mitandaoni na kwamba utapeli na rushwa ni matukio mabaya ambayo wastaafu wengi wamekutana nayo na kuwataka kuchukua tahadhari zote za kukabiliana nayo.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Mahakama ya Tanzania, mkoa wa Morogoro ndugu Nestory Mujunangoma amewataka washiriki hao kufanya maandalizi ya kustaafu mapema na kuchukua maamuzi sahihi ambayo hayataathiri maisha yao baada ya kustaafu huku akilinganisha kustaafu kama kubadili gia kwenye gari na kwamba maisha yanaendelea hata baada ya kustaafu kama ambavyo gari huendelea hata baada ya kubadili gia.
Naye Mratibu wa Mafunzo hayo Ndugu Nuhu Mtekele, Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto aliewaeleza washiriki hao kuwa mafunzo hayo ni mpango wa utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2013, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019 pamoja Mpango Mkakati wa Chuo wa miaka mitano wa mwaka 2018/19-2022/23.
Ndugu Mtekele aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na mafunzo ya darasani, washiriki watapata fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro ili kujionea kwa vitendo miradi na shughuli za ujasiriamali na uwekezaji katika nyanja za kilimo na ufugaji na zile ambazo wanaweza kupenda kuzifanya na hatimaye kuwasaidia kimaendeleo baada ya kustaafu.
Mafunzo hayo yameratibiwa na kuendeshwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Mafunzo hayo yamejumuisha washiriki wa kada mbalimbali wakiwepo mahakimu, wasaidizi wa kumbukumbu, makatibu mahususi, walinzi n.k.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo akifungua rasmi mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwa Watumishi wa Mahakama ya Tanzania ambao hawapo pichani
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kustaafu.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kustaafu.
Picha mbalimbali za washiriki wa Mafunzo ya Kujiandaa kustaafu wakiwa wanafualitia ufunguzi wa mafunzo hayo ulifanyika katika ukumbi wa Magadu Mkoani Morogoro
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Mahakama ya Tanzania Bwana Edward J.K. Nkembo (aliyeketi katika) kulia kwake ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Morogoro Ndugu Nestory C. Mujunangoma na kushoto ni Ndugu Nuhu Mtekele Mhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mratibu wa Mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na sekreatieti.
0 comments:
Post a Comment