Na: Rosena Suka, IJA
Leo tarehe 24 Februari, 2024 ujumbe wa Benki ya Dunia umetembelea mradi wa ujenzi wa studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ unaofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Mradi huo ni kati ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mahakama ya Tanzania kwa ufadhili wa Benki wa Benki ya Dunia.
Ziara hiyo imewakilishwa na Maafisa wanne kutoka Benki ya Dunia ukiwa unaongozwa na Bi. Christine Owuor na Maafisa wengine watatu. Pamoja na Maafisa hao pia kulikuwa na watumishi kadhaa wa Mahakama ya Tanzania akiwemo Jaji Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.
Baada ya kuwasili Chuoni ujumbe huo ulifika katika eneo la Mradi wa ujenzi wa Studio jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ ambao umeanza tarehe 18 Februari, 2024 na unategemea kumalizika tarehe 18 Mei.
Ujumbe huo pia ulipata maelezo ya uundwaji na matumizi ya studio hiyo itakavyo fanya kazi kutoka kwa Mhandishi Emmanuel Mbosso wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo. Pia alieleza kwa ugeni kuwa Jukwaa la kujifunzia mtandaoni limetengenezwa na wataalamu wa ndani ya Tanzania ambao ni kutoka Mahakama ya Tanzania, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo cha Serikali za Mitaa (Hombolo).
Jukwaa la mafunzo ya mtandao litarahisisha utoaji wa mafunzo kwa watumishi wengi wa mahakama, kwa gharama nafuu na kupunguza umbali wa kufuata mafunzo.
Picha ya pamoja ya Maafisa wa Benki ya Dunia waliotembelea mradi wa ujenzi wa studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ unaofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Waliokaa katika ni Bi. Christine Owuor ambaye Kiongozi wa Ujumbe kutoka Benki ya Dunia. Kushoto ni Jaji wa Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo na Kulia ni Jaji Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha. na waliosimama nyuma ni Maafisa wa Benki ya Dunia.
Picha ya juu na ya chini ni watumishi wa IJA na Mahakama waliokuwa kwenye mapokezi ya ugeni wa wakilishi wa Benki ya Dunia wakifuatilia taarifa mbalimbali zilizokuwa zinatolewa kuhusu mradi ujenzi wa wa studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ unaofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mhandishi Emmanuel Mbosso wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo akitoa maelezo ya uundwaji wa studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’
Picha ya juu na chini ni Wajumbe wa Benki ya Dunia na Viongozi wa Mahakama ya Tanzania wakipata maelezo ya mradi wa ujenzi studio ya jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’ kutoka kwa Mhandisi wa mradi huo.
Meza kuu na viongozi kutoka Mahakama ya Tanzania
Meza Kuu na Sekretarieti
Meza kuu na Baadhi ya watumishi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
Meza Kuu na baadhi wa watalaamu walioshiri kutengeneza jukwaa la kufundishia kwa njia ya mtandao ‘e-learning’
0 comments:
Post a Comment