Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto leo tarehe 9 Agosti, 2022 amefungua mafunzo ya siku tano kwa Makatibu Mahsusi wapatao 56 wa Mahakama ya Tanzania yanayohusu Namna Bora ya Uendeshaji wa Ofisi. Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 09 Agosti ,2022 mpaka 13 Agosti, 2022 katika ukumbi wa Mafunzo uliopo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Akifungua mafunzo hayo Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo amewataka Makatibu
Muhtasi kutoa huduma bora zinazoendana
na uwekezaji katika majengo ya Mahakama nchini. Aliendelea kwa kusema kuwa, Mahakama
ya Tanzania iko katika maboresho ambayo yanagusa maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu
ya majengo na raslimali watu hivyo mafunzo haya yana lengo la kuwaandaa
watumishi hao ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea.
“Hivyo lengo la mafunzo yanayotolewa ni kujaribu kuwajengea uwezo na kubadilisha fikra za watumishi wa Mahakama ili huduma wanazozitoa mahakamani ziendane na ubora wa majengo ambayo yanaendelea kuboreshwa,” amesema.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania, Bi.
Beatrice Patrick amewaambia washiriki hao kuwa Mahakama imejipanga kuwajengea
uwezo watumishi wake katika kada mbalimbali ili kuendana na maboresho
yanayoendelea.
Bi. Beatrice Patrick
amesema kundi hilo la washiriki wa mafunzo linajumuisha Makatibu Muhtasi 56,
ambapo 50 wametoka katika Mahakama mbalimbali za Mwanzo, Mahakama za Wilaya na
Mahakama za Hakimu Mkazi, washiriki sita wakiwa ni waajiriwa wapya.
Amesema kuwa watumishi hao wanapewa mafunzo hayo kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi za Ukatibu Muhtasi, utunzaji wa kumbukumbu, usimamizi wa ofisi na mawasiliano ya kiofisi, uzalendo na protokali, mipango ya Mahakama na uboreshaji, huduma kwa mteja, masuala ya saikolojia na ushauri, mwelekeo wa Mahakama kwa sasa katika mapinduzi ya viwanda kuelekea Mahakama Mtandao na matumizi ya TEHAMA.
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akisisitiza jambo alipokuwa anafungua mafunzo ya
siku tano kwa Makatibu Muhtasi 56 yaliyoanza kufanyika leo tarehe 9 Agosti,
2022.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick
akizungumza kwa ufupi kumkaribisha Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul
Kihwelo kufungua mafunzo hayo.
Sehemu
ya Makatibu Muhtasi wanaoshiriki katika mafunzo (picha mbili juu na moja chini)
ikifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mkuu wa Chuo.
Meza
Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na
Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (katikati) ikiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wote wa mafunzo.
Meza
Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na
Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (katikati) ikiwa katika
picha ya pamoja na Mahakiumu wa Mahakama za Lushoto waliohudhuria kwenye ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya mafunzo










.jpeg)

0 comments:
Post a Comment