Mhe. Amiri Mruma, Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam amefungua mafunzo ya uendeshaji wa mashauri Makosa ya Kifedha (Financial Crimes) kwa maafisa
wa Mahakakama 30 katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo ya
siku tano kuanzia leo tarehe 07/11/2022 yameandaliwa na Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Eastern and
Southern Africa Anti-Money Laundering Group (ESAAMLG) na Shirika la
Maendeleo la Ujerumani (GIZ).
Washiriki wa mafunzo hayo ni
Majaji 14 pamoja na Mahakimu Wakazi 26 ambapo kati yao 24 ni Mahakimu Wakazi wa Mikoa Tanzania
Bara. Lengo la mafunzo hayo ni kuwafanya washiriki hao waweze
kubadilishana uzoefu kwenye maeneo mbalimbali ya sheria za kimataifa na kitaifa za biashara haramu ya wanyamapori, ufadhili wa ugaidi
na utakatishaji fedha, kuangalia madhara ya makossa hayo katika taifa na dunia,
urejeshaji wa mali zilizopatikana kutokana na
makosa hayo, wajibu wa Maafisa wa Mahakama, wapelelezi na waendesha mashtaka
katika uendeshaji wa mashauri yahusuyo makosa hayo n.k.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo
ni baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ofisi ya Mashtaka ya Taifa, Wizara
ya Maliasili na Utalii, PPRA, wawezeshaji kutoka mamlaka za wanyamapori za baadhi
ya nchi barani Afrika na wawezeshaji wabobevu kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mafunzo haya ni muendelezo
wa mafunzo mengine kama
hayo yaliyotolewa kwa kundi la kwanza la Mahakimu 40 mwezi Septemba mwaka huu.
Pichani juu Mhe. Amiri Mruma, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam (katikati) alipokuwa anafungua mafunzo ya mafunzo ya uendeshaji wa mashauri Makosa ya Kifedha (Financial Crimes) kwa maafisa wa Mahakama kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara ambao wanaonekana kwenye picha za chini.






0 comments:
Post a Comment