Na Rosena Suka, IJA
Mhe. Dkt. Gerald Ndika, Jaji wa Mahakama ya
Rufani Tanzania leo Desemba 6, 2022 amefungua Kongamano la Kitaaluma lililoandaliwa
na Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA ALUMNI)
katika ukumbi wa Barnabas Samatta Chuoni Lushoto.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Mhe. Dkt.
Ndika alianza kwa kuwapongeza wanajumuiya hao kwa kujitolea na kushiriki katika
shughuli mbalimbali zenye nia ya kutoa elimu na kukuza uelewa katika jamii
kuhusiana na masuala ya sheria ikiwepo kuandaa makongomano ya kitaaluma kama
hilo, kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi bure na kushiriki katika masuala
mbalimbali yanayoandaliwa na Chuo kwa lengo la kuwaunganisha na kuwajengea
umoja wahitimu wote wa chuo.
Mhe. Dkt. Ndika aliendelea kwa kusema
kongamano hilo ni fursa nzuri kwa washiriki kudadavua masuala muhimu yahusuyo
mambo mbalimbali ya kiuchumi na ya kijamii, sambamba na kuangalia ukuaji katika
maeneo ya utoaji haki.
“ Na ni mategemeo ya Chuo na Taifa
kwa ujumla kwamba kila mmoja wenu mara baada ya kuhitimu kwenu mnapaswa kuelewa
kwamba nafasi nliyonayo ni vema mkaitumia katika kuleta maendeleo ya nchi na
jamii kwa ujumla ili kukuza taaluma na kuielimisha jamii katika utoaji haki,
mkizingatia usawa, Amani na usalama” alisema Mhe. Dkt. Ndika.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo na Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo akiwa anafunga kongamano hilo aliwahimiza
washiriki wa kongamano kutumia fursa
hiyo ili kuwa na mahusiano mazuri na kuitumia Jumuiya ya Wahitimu hao ili
kupata fursa mbalimbali za kujifunza katika taaluma waliyonayo.
Kongamano hilo lililowashirikisha wanachuo wote lililoongozwa na mada isemayo “IJA and Prospects for offering practical legal training to lawyers Employed in Public Service ; Practicalities and Challenges” na hufanyika mara moja kila mwaka siku moja kabla ya sherehe za mahafali ya Chuo.






0 comments:
Post a Comment