Leo
tarehe 6 Machi, 2023 Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Waziri wa Katiba na
Sheria amefanya ziara ya siku moja katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
kwa kutembelea maeneo mbalimbali na kuona shughuli zinazofanyika chuoni na alipata
wasaa wa kuongea na Menejimenti ya Chuo na Watumishi katika ukumbi wa mafunzo
wa Ibrahim Hamis Juma. Katika ziara hjyo
Mhe. Dkt. Ndumbaro ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Dkt. Khatibu Kazungu
Akizungumza
na Menejimenti na Watumishi Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa salamu za pongezi kwa
Chuo kwa kufanya majukumu yake ya msingi kama sheria ya uanzishwaji wake
ilivyotaka. Kwani kwa sasa Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto ndicho Chuo pekee kilichobaki kwenye misingi yake hapa
Tanzania.
Aliendelea
kwa kusema kwamba, uimara na ubora wa Mhimili wa Mahakama umetokana na ubora
Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kutoa mafunzo ya kujengea uwezo
watumishi wa Kada mbalimbali wa Mhimili wa Mahakama na wadau wengine wa Sheria
nchini, hivyo amekitaka Chuo kupanua wigo nje ya mipaka ya Tanzania ili
kujipatia sifa chenyewe, Mhimili wa Mahakama na Tanzania kwa ujumla.
Mhe.
Dkt. Ndumbaro aliendelea kwa kutoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa bidii na
kuheshimu haki na misingi ya mtumishi wa umma katika utendaji wa kazi zao za
kila siku. Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema “Utumishi wa Umma unaongozwa na Katiba, Miongozo na mila na desturi” alisema Mhe. Dkt.
Ndumbao.
Naye
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Dkt.
Gerald A. Ndika katika salamu zake amemshukuru Mhe. Dkt. Ndumbaro na Dkt.
Kazungu kwa kufanya ziara hiyo ya kutembelea Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto. Mhe. Dkt. Ndika aliendelea kwa
kusema kwamba matarajio ya Mhimili wa Mahakama kwa Chuo yamefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kwa Chuo kuwa kitovu cha mafunzo ya watumishi wa mahakama na Chuo
kimekuwa kikitoa machapisho mbalimbali yanayosaidia katika utendaji kazi wa
kila siku wa watumishi wa mahakama hususani Majaji na Mahakimu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Dkt. Paul F.
Kihwelo alisema Chuo kwa sasa kinaendesha mafunzo mbalimbali ya kuwajengea
uwezo watumishi wa mahakama ili kuendana kasi ya Mhimili wa Mahakama. Na aliendelea
kwa kusema Chuo kimefanya mafunzo mengi ya aina mbalimbali kwa njia ya mtandao,
kwakufanya mafunzo kwa njia imekuwa ikitoa mafunzo idadi kubwa ya watumishi wa mahakama na kwa wakati hivyo kupelekea Mahakama kupunguza mzigo mkubwa bajeti ya mafunzo kwa
watumishi.
Mhe.
Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kusema Chuo kimekuwa kikifanya vizuri katika utoaji
wa mafunzo toka kilipoanzishwa na kupelekea wahitimu wengi kupata teuzi
mbalimbali na kuajiriwa katika taasisi mbalimbali za utoaji haki na Mhimili wa
Mahakama.
0 comments:
Post a Comment