Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson amezindua maadhimisho ya wiki ya sheria leo tarehe 27 Januari, 2024 katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo Mhe.
Dkt. Tulia alikuwa mgeni rasmi wa
shughuli hiyo na amewataka washiriki wa maonesho hayo kuelimisha wananchi kwenye
mambo mbalimbali yahusuyo sheria.
Sambamba na uzinduzi wa wiki ya sheria, Mhe. Dkt. Tulia pia amezindua rasmi Mfumo wa Udukuzi na Tafsiri (TTS) wa Mahakama ya Tanzania ambao utatumika katika kutafsiri na kunukuu lugha zinazotumika mahakamani mbazo ni Kiswahili na Kingereza na utakaorahisisha zaidi huduma ya upatikanaji haki kwa wananchi.
‘‘Naamini
kazi kubwa sasa, hasa wadau wa Mahakama ni utengenezaji wa mfumo hasa wa
kitehama, utakaowasaidia wadau hawa kufungamanisha na kuboresha Mfumo Jumuishi
wa Haki Jinai unaosomana, ili kubadilishana taarifa kuanzia hatua ya upelelezi,
ufunguaji wa mashauri, msaada wa kisheria, uendeshaji wa mashtaka, kusikiliza
mashauri na utoaji uamuzi,” amesema Mhe. Dkt. Tulia.
Mhe. Prof. Juma aliendelea kwa kueleza faida za mfumo huo kuwa utawaapunguzia kazi Majaji na Mahakimu waliyokuwa wanaifanya ya kuandika kwa mkono mienendo ya mashauri kwa mfumo huu utarahisha na kufanya wananchi kupata haki kwa wakati.
Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto ni miongoni mwa Wadau mbalimbali wa Mahakama, ambapo wanashiriki katika
Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza tarehe 24 Januari mpaka 30 Januari,
2024. Wadau wengine wa Mahakama wanaoshiriki katika maonesho hayo ni Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa
ya Mashtaka, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Tume ya Haki za Binadamu, Chama
cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA), Polisi, Magereza na Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS).
Katika maadhimisho haya ya Wiki
ya Sheria na Siku ya Sheria, kauli mbiu ni “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa:
Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai.
Maonesho haya
yaliyozinduliwa leo yatafanyika kwa muda wa siku nane ambapo yanatarajiwa
kukamilika tarehe 30 Januari, 2024 ambapo yatahitimishwa kwa kilele cha Siku ya
Sheria itakayofanyika tarehe 01 Februari, 2024 na mgeni rasmi wa siku hiyo
anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan.
Viongozi wakiwa katika matembezi maalum kwa ajili ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika tarehe 27 Januari, 2024 katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma.
Jaji wa Mahakama Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria uliofanyika tarehe 27 Januari, 2024 katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson(katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho wiki ya sheria,
Baadi ya washiriki wa maonesho ya Wiki ya Sheria wakiwa wanafuatilia uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Sheria uliofanyika tarehe 27 Januari, 2024 katika Viwanja vya Nyerere ‘Square’ jijini Dodoma
0 comments:
Post a Comment