Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman leo tarehe 18 Januari, 2022 amefungua mafunzo elekezi kwa Mahakimu Wakazi wapya thelathini na tano. Mafunzo haya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto yatafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 18 Januari mpaka 22 Januari, 2022. Mahakimu hawa ni wale walioteuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahimu Hamis Juma tarehe 17 Januari, 2022.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo hayo, Jaji Mkuu Mstaafu aliwaambia Mahakimu hao kuwa
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ni ngazi ya uongozi na hivyo wanaingia
kwenye mahakama ya mwanzo kama viongozi kwa
mategemeo ya kuongoza watumishi watakaofanya nao kazi waliochini yao. Pia aliongeza kuwa mahakama
inawategemea katika kusimamia mpango mkakati na maboresho ya mahakama ili
kuleta mabadiliko chanya ndani ya Mahakama.
Mhe.
Othman aliwasisitiza Mahakimu hao kuwa taswira ya Mahakama ya Mwanzo kwa sasa
imebadilika sana na hivyo wao pia waendelee kuibadilisha na kuifanya bora zaidi
ili huduma kwa wananchi ziwe bora zaidi na kwa wakati.
“Mahakama za mwanzo ndio zinatoa fursa kubwa
zaidi kwa Watanzania kupata haki kuliko mahakama nyingine zote kwa sababu
zimetapakaa Tanzania nzima”, alisema Mhe. Othman.
Hata
hivyo Mhe. Othman hakusita kuwakumbusha mahakimu hao kuwa makini kwenye nguzo
muhimu ya uhuru wa kila hakimu na uhuru wa mahakama. Aliwasisitiza kuamua mashauri
yaliyo mbele yao kwa sheria bila woga wala shinikizo.
“Watanzania
wanataka Mahakama huru, inayotoa haki kwa wakati, mahakama adilifu, Mahakama
ambayo ina uwezo na Mahakama ambayo haina gharama kubwa” aliongeza Mhe. Othman.
Mhe.
Othman aliwaasa Mahakimu hao kujua na kufuata taratibu zilizowekwa na mahakama
wakati wa uendeshaji wa mashauri hadi wanapofikia kutoa maamuzi ikiwemo taratibu
za usikilizaji wa shauri na kutoa uamuzi unaoongozwa na sheria pamoja na kuweka
sababu za hukumu bila kusahau kupata maoni kutoka kwa wazee wa baraza.
Kwa
upande wake Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa
Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto ni kitovu cha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa kada mbalimbali
wa Mahakama na wadau wa sheria
nchini.
Mhe.
Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kusema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Mafunzo ya
Taifa ya 2013 na Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2021/22-2024/25, Sera
ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya mwaka 2019 ambayo inaelekeza kila mtumishi anayeajiriwa, kupanda cheo au
kuteuliwa kabla hajaanza majukumu mapya apate mafunzo elekezi kwa lengo la
kuboresha huduma za mahakama.
Mhe.
Dkt. Kihwelo alielezea Mahakimu hao kuwa Chuo kina Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mwaka 2018/19-2022/23, na
eneo ambalo chuo limekuwa likijizatiti ni eneo la mafunzo ya aina hiyo ya kuwajengea
uwezo watumishi wa mahakama.
Mhe.
Dkt. Kihwelo aliendelea kwa kuwaomba Mahakimu wajitahidi sana kutoa huduma
nzuri na kujiepusha na rushwa kwani kwa sasa mahakama zimeboreshwa kwa kuwa na
majengo mazuri sana na hivyo basi huduma ziendane na majengo.
Wakati
huohuo, Mhe. Sharmillah Sarwat, Msajili
wa Mahakama Kuu ya Tanzania ameupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa
programmu za maboresho yanayaofanyika ikiwepo kuwekeza kwenye raslimali watu ambapo Chuo kimekuwa ikifanya kwa vitendo kuwajengea uwezo
watumishi hao wa Mahakama wakiwemo Mahakimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao
kwa ufanisi na weredi.
1. Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji, Mkuu Mstaafu
wa Mahakama ya Tanzania akifungua Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi
Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mhe. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akiwa anawakaribisha washiriki Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
1. Mhe. Sharmillah Sarwat
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania akitowa utambulisho kwenye Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto
1. Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu
Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa
wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe.
Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
1. Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu
Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa
wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe.
Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
1. Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu
Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa
wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe.
Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
1. Washiriki wa Mafunzo Elekezi kwa Mahakimu
Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.wakiwa
wanafuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kutoka kwa Mhe.
Mohamed Chande Othman (hayupo pichani)
1.
Mhe. Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu Mstaafu
wa Mahakama ya Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji Mafunzo Elekezi
kwa Mahakimu Wakazi Wapya yanayoendeshwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto
2.
3.
0 comments:
Post a Comment