Na Rosena Suka, IJA
Kaimu Mkuu wa Chuo na Naibu
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Taaluma, Tafiti na Ushauri,
Bw. Goodluck Chuwa leo tarehe 14 Desemba, 2023 amefungua mafunzo elekezi ya siku moja kwa Viongozi wa Serikali ya
Wanachuo wa IJA (IJASO) kwa mwaka wa
masomo 2023/2024 yaliyofanyika Chuoni Lushoto.
Kwenye ufunguzi huo Bwana Chuwa amewaeleza viongozi
hao kwamba lengo kuu la
mafunzo hayo elekezi ni kuwajengea uwezo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya uongozi kwa kufuata miongozo
ya sheria, taratibu na kanuni za chuo na taifa kwa ujumla.
Bwana Chuwa
aliendelea kwa kusema viongozi hao wamebeba dhamana kubwa ya kuwahudumia wanachuo
wenzao kwa sababu wao ni
kiungo katika kuwafikisha maelekezo yote yanayotolewa na Menejimenti kwenda
kwa wanachuo na kutoa mrejesho kutoka kwa wanaowangoza kuja kwenye menejimenti bila
kuongeza au kupunguza uhalisia.
Naye Makamu
Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Fatihiya Massawe aliwasisitiza
viongozi hao wa wanachuo kutendea haki nyadhifa
walizonazo kwa kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili waliowachugua kwani serikali ya wanachuo ni chombo muhimu katika
musitakabali wa Chuo.
Prof. Masawe
aliwakumbusha viongozi hao kusimamia sheria, kanuni na taratibu zilizopo ili kuonyesha
mfano bora kwa wanachuo wenzao.
Katika semina hiyo
elekezi viongozi hawa wamepitishwa katika mada mbalimbali zilizotolewa na
watoa mada kutoka katika taasisi za umma Wilayani Lushoto ambao ni Mwakilishi
kutoka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (PCCB), Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi
na Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Mada nyingine zilitolewa na vitengo na Idara vya
ndani ya Chuo ambavyo ni Mkaguzi wa ndani, Mhasibu Mkuu,Mdhibiti ubora, Msajili
na Mshauri wa Wanachuo.
Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto kina utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kwa Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kila mwaka mara tu serikali hiyo inapowekwa madarakani.
Kaimu Mkuu wa Chuo na Naibu Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Taaluma, Tafiti na Ushauri, Bw. Goodluck Chuwa akifungua Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO
Naibu Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Fatihiya Massawe akiwaelekeza Viongozi wa Serikali ya Wanachuo katika Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO
Mwakilishi kutoka Taasisi ya Kupambana na Rushwa Wilayani Lushoto (PCCB) Bwana Norbert Massaba akiwasilisha mada kwa Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwenye Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO
Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwenye Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO wakifuatilia mada
Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwenye Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO wakifuatilia mada
Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwenye Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO wakifuatilia mada
Viongozi wa Serikali ya Wanachuo kwenye Mafunzo Elekezi kwa Serikali ya Wanachuo IJASO wakifuatilia mada
0 comments:
Post a Comment