Wanachuo 50 wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto(IJA) leo Mei, 4 2023 wamefanyia ziara ya kimasomo ya siku moja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Sambamba na ziara hiyo wanachuo hawa wamepata fursa ya kutembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Morogoro walipokuwa safarini kuelekea Dodoma ambapo kwenye kituo hicho walipata fursa ya kuona shughuli mbalimbali za kimahakama zinavyoendeshwa.
Wakiongea baada ya ziara yao Bungeni wanachuo hao wa IJA wameupongeza Uongozi wa Chuo, watumishi wa kituo Jumuishi cha Mahakama Morogoro kwa kufanikisha ziara hiyo.
Pia wametoa shukrani nyingi kwa Mbunge wa Lushoto Mhe. Shaban Shekilindi Kwa kuwa mwenyeji wao walipotembelea bungeni kwa kusema kwamba wamepata mafanikio makubwa na wamejifunza mambo mengi kuhusu mwenendo wa Bunge pamoja ma historia ya bunge hilo.
Wanachuo hao wakiwa wameambatana na walezi wao wa Chuo Bi. Frida Nicholaus na Bw. George Banoba kesho tarehe Mei, 5 2023 watapata nafasi nyingine ya kutembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Dodoma.
Picha mbalimbali za Wanafunzi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge walipofanya ziara Bungeni Jijini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment